Mwezi kumi na tatu Rajabu Ulimwengu uliangaziwa na Nuru ya kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s).

Maoni katika picha
Katika siku kama leo mwezi kumi na tatu Rajabu, miaka thelathini baada ya tukio la watu wa tembo, Dunia ilinawirika kwa kuzaliwa Quráni yenye kutamka Mbora wa mawasii kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), aliye zaliwa ndani ya Kaaba tukufu, hakuwahi kuzaliwa kabla yake wala hata tokea baada yake mtu kuzaliwa ndani ya Alkaaba Zaidi yake, hiyo ni heshima na utukufu aliopewa na Mwenyezi Mungu (s.w.t).

Kutoka kwa Saidi bun Jubair anasema: Yazidi bun Qa’nab anasema: Nilikua nimekaa pembeni ya nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu na Abbasi bun Abdulmutwalib pamoja na kundi la watu wa Abdul Uza, akaja Fatuma binti Asadi mama wa kiongozi wa waumini (a.s), alikua na ujauzito wa miezi tisa, akiwa amepata uchungu, akasema: Mola wangu Mlezi! Mimi nakuamini na ninaamini kila kilicho toka kwako miongoni mwa Mitume na vitabu, ninasadikisha maneno ya babu yangu Ibrahim Khaliil, na ndiye aliyejenga nyumba hii tukufu, kwa utukufu wa aliyejenga nyumba hii na utukufu wa mototo aliye tumbani kwangu nakuomba unifanyie wepesi katika uzazi wangu.

Yazidi bun Qa’nab anasema: Nyumba ikapasuka na Fatuma akaingia na kutoweka katika macho yetu, halafu ukuta ukaungana, tukaenda kufungua kufuli la mlango halikufunguka, tukatambua hiyo ni amri ya Mwenyezi Mungu mtukufu, kisha akatoka baada ya siku nne akiwa amemshika kiongozi wa waumini (a.s), halafu akasema: mimi nimetukuzwa juu ya wanawake walio nitangulia, Asia bint Muzaahim alimuabudu Mwenyezi Mungu kwa siri katika sehemu ambayo ilikua ni marufuku kuabudiwa Mwenyezi Mungu na yeyote mwenye kumuabudi anapewa adhabu kali, na Maryam bint Imraan alitikisa mtende mbichi ukadondosha tente zilizowiva vizuri, na mimi nimeingia katika nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu na nimekula matunda ya peponi, nilipo taka kutoka nikasikia sauti ikiniambia: Ewe Fatuma mwite Ali ni Ali, na Mwenyezi Mungu ni Aliyyul A’laa, sauti ikasema: nimetoa jina lake katika jina langu, na nimemfundisha adabu zinazo tokana na mimi, atazama katika elimu, na atavunja masanamu katika nyumba yangu, na ataadhini juu ya nyumba yangu, atanitakasa na kunitukuza, amefaulu atakaye mpenda na kumtii, na ole wake atakaye muudhi na kumuasi.

Yatupasa kukumbusha kua fadhila na utukufu wa Imamu Ali (a.s) wa kuzaliwa ndani ya Alkaaba, hakuna mtu yeyete aliye upata katika historia ya mwanaadamu, Ali (a.s) ni mtu wa kwanza kuzaliwa ndani ya Alkaaba, na hatazaliwa mwingine baada yake, hiyo ni heshima ya pekee aliyopewa na Mwenyezi Mungu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: