Shamra shamra za kuadhimisha kuzaliwa kwa kiongozi wa waumini (a.s) zimeenea jirani na malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na kufanyika kongamano la washairi.

Maoni katika picha
Katika mazingira yaliyojaa shangwe na furaha jirani na malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kuadhimisha mazazi ya kiongozi wa waumini Imamu Ali (a.s), kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu kinafanya hafla kubwa na kongamano la ushairi, ambalo limehudhuriwa na washairi wengi, pamoja na kundi kubwa la mazuwaru kutoka ndani na nje ya Karbala.

Hafla hiyo imefunguliwa kwa Quráni tukufu, halafu ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kisha yakafuata mashairi mbalimbali na kaswida za kishairi, zilizo elezea mapenzi yao kwa Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s), na namna wanavyo shikamana na kiongozi wao Ali bun Abu Twalib (a.s), na kufuata mwenendo wake pamoja na mwenendo wa kizazi chake, na kushikamana nao sambamba na kuhuisha mafundisho yao jambo linalo ingiza furaha kwa Imamu wa zama (a.f).

Kumbuka kua idara ya matangazo katika kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu, imezowea kufanya kongamano hili kila mwaka, pamoja na kongamano la kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume (s.a.w.w), na tarehe za kuzaliwa maimamu watakasifu na Idul-Ghadiir, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha alama za Dini zenye athari kubwa kwa waumini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: