Miongoni mwa mambo yaliyopo katika ratiba ya kongamano na maonyesho ya pili ya ubunifu, yanayo fanywa chini ya kauli mbiu isemayo: (Karbala ni kitovu cha elimu na wanachuoni) linalo endeshwa na muungano wa wabunifu wa kiiraq, chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ni kufanya kikao cha kitafiti kilicho elezea moja ya bunifu zinazo shiriki katika maonyesho haya, kikao hicho kimefanyika asubuhi ya siku ya Alkhamisi (13 Rajabu 1440h) sawa na (21 Machi 2019m) katika ukumbi wa mikutano ndani ya jengo la Shekh Kuleini (r.a) na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya watafiti.
Kikao kimeongozwa na Ustadh Zaiduni Khalfu Saidiy, khutuba ya utambulisho imetolewa na kiongozi mwandamizi wa kituo cha masomo na utafiti Alkafeel ambacho kipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Swafaa Mussawi, ameeleza kazi inayofanywa na Ataba tukufu katika kusaidia mambo ya kitaifa kwenye sekta tofauti, ameelezea pia miradi ya Ataba tukufu, kuanzia iliyo fanywa ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na miradi ya kilimo, viwanda, afya, ujenzi, utumishi, utamaduni na elimu.
Ukafuata muhadhara ulio tolewa na makamo mkuu wa muungano wa wabunifu wa kiiraq Dokta Abduljaasim Muhisan Jaasim, ambaye ameeleza namna muungano huo unavyo saidia wabunifu wa kiiraq kwenye mahafali ya kitaifa na kimataifa, jambo ambalo limewawezesha kuchangia mafanikio mengi.
Kisha ukaingia wakati wa wabunifu wanaoshiriki kwenye kongamano hili na ambao ubunifu wao umepata nafasi ya kushiki katika maonyesho, mada ya kwanza ikawa ya kitabibu yenye anuani isemayo (Utengenezaji wa viungo bandia), kutoka chuo kikuu cha Mustanswariyya, iliwasilishwa na Dokta Kaadhim Kaamil Rasan. Mada ya pili ikawa ya kihandisi yenye anuani isemayo: (Zana za ujenzi za G.R.P haziwezi kutoweka) iliyo wasilishwa na Mhandisi wa kiiraq Abdulatifu Muhammadi.