Maoni katika picha
Mjumbe katika wageni wa Ataba, Shekh Muhsin Asadiy amesema kua: “Hakika ni fursa nzuri ya kushirikiana na binti zetu wa wilaya ya Swawira katika hafla hii, kutokana na umuhimu wa umri wa kubalekhe kwa wasichana na wavulana, huu ni umri muhimu sana katika uhai wao, wamejiandaa vipi kimwili na kiakili katika kukabiliana na mabadiliko makubwa na muhimu katika uhai wao, mabadiliko ya kutoka katika hatua ya utoto na kuingia katika hatua ya ukubwa, hatua ya makuzi na mitihani katika maisha, hafla hii ni uzinduzi kwa kila kijana wa kumtaka awajibike katika kutekeleza majukumu aliyo pewa katika maisha yake”.
Akaongeza kua: “Tuliandaa zawadi za mabinti ambao walikua zaidi ya mia moja, wamepewa vitambaa vya kutabaruku na malalo ya Abulfadhil Abbasi pamoja na vipeperushi vya mafundisho na maelekezo mbalimbali yanayo endana na umri wao wa sasa na siku zijazo”.