Wingu la furaha za Alawiyya latanda katika Atabatu Abbasiyya.

Maoni katika picha
Dunia haitambui mtu mwenye fadhila ukaribu na tabia njema baada ya Mtume (s.a.w.w) kama alivyokua kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), amewashinda watu wa mwanzo na hakuna atakaye mfikia, utukufu wake (a.s) ni mwingi sana hauelezeki, unawezaje kuhesabu utukufu wa mtu ambaye Mtume (s.a.w.w) katika siku aliyo pigana na Omari bun Abdul Wudi Al-Aamiriy alisema: (Imepigana Imani yote dhidi ya ukafiri wote), na baada ya Imamu kumuua Omari bun Abdul Wudi Mtume akasema: (Pigo la Ali kwa Omari siku ya Khandaki ni sawa na ibada ya vizito viwili).

Katika kuadhimisha na kukumbuka kuzaliwa kwake Malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imepambwa kwa ajili ya maadhimisho haya, imejaa shangwe na furaha, shamba boy wa Alkafeel chini ya kitengo cha utumishi wamepamba haram tukufu ndani na nje kwa kuweka maua ya aina mbalimbali, kwa ajili ya kuingiza furaha katika nyoyo za wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s), na kuwafanya waishi katika mazingira wa furaha, kwa kuweka mazingira yanayo endana na tukio hili, katika milango ya Atabatu Abbasiyya tukufu na katika korido za haram na pembezoni mwake, hadi katika uwanja wa katikati ya haram mbili kumewekwa aina nzuri za maua.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: