Malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imefurika makundi ya mazuwaru.

Maoni katika picha
Malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) baada ya Adhuhuri ya siku ya Alkhamisi (13 Rajabu 1440h) sawa na (21 Machi 2019m) imeshuhudia idadi kubwa ya mazuwaru, japokua imezoweleka kuwa na mazuwaru wengi kila usiku wa Ijumaa, lakini leo ni tofauti na siku zingine kutokana na wingi wa mazuwaru waliojitokeza, siku ya leo ni siku tukufu sana kwa kuadhimisha kuzaliwa kwa baba yake kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), watu wamekuja kufanya ziara kwa Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na kumpongeza kwa tukio hili adhim, utakuta mazuwaru wanapongezana huku wanakwenda katika kaburi tukufu kwa ajili ya kutoa pongezi zao za dhati kufuatia maadhimisho haya.

Mazuwaru wengi wamekuja kutoka Najafu, baada ya kumaliza ziara kwenye malalo takatifu ya kiongozi wa waumini (a.s).

Kama kawaida ya Atabatu Abbasiyya tukufu kila usiku wa Ijumaa hufungua milango yake kwa ajili ya kupokea mazuwaru watukufu, wanaokuja kwa Abulfadhil Abbasi (a.s) kutoka sehemu tofauti, mawakibu za kutoa huduma pia zimeweka mahema bembezoni mwa barabara na katika viwanja vya umma pamoja na kwenye husseiniyyaat mbalimbali na kutoa huduma ya chakula na vinywaji kwa mazuwaru watukufu.

Kamera ya Alkafeel imeshuhudia harakati za mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s) na inakuletea baadhi ya picha zao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: