Kutokana na muendelezo wa ziara zake zilizo pita na kukamilisha miradi wanayo tekeleza katika malalo ya bibi Zainabu (a.s), ujumbe wa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu umewasiri katika mji mkuu wa Sirya Damaskas, kwenye malalo ya bibi Zainabu (a.s), kwa ajili ya kuomboleza kifo chake kilicho tokea mwezi kumi na tano Rajabu, pamoja na kutoa huduma mbalimbali katika haram hiyo na kwa mazuwaru watukufu.
Kuhusu ziara hii tumeongea na rais wa ujumbe huo bwana Hassan Hilali, ambaye pia ni rais wa usimamiza wa haram kutokana na maelekezo ya Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ametuambia kua: “Atabatu Abbasiyya tumekuja katika haram ya Aqilah Zainabu (a.s) kutoa huduma ndani ya haram na kwa mazuwaru kwa mara ya sita, safari hii tumechagua kuja katika mwezi wa Rajabu katika siku za kuomboleza kifo cha bibi Zainabu (a.s), kuweka mapambo meusi na kuwasha taa nyekundu ndani ya korido za haram tukufu, sambamba na kutoa huduma katika sekta tofauti, sekta ya umeme, ujenzi na zinginezo…, hadi baada ya kumaliza kipindi cha ziara ya kuomboleza kifo chake”.
Akaongeza kua: “Kuna ushirikiano mkubwa kati ya Atabatu Abbasiyya na ndugu zetu katika Atabatu Zainabiyya, kwa ajili ya kuwahudumia mazuwaru watukufu, na kuiweka haram katika mazingira mazuri, katika safari iliyo pita tuliandika mahitaji yoto ya haram yaliyotajwa na ndugu zetu watumishi wa Atabatu Zainabiyya, safari hii tumekuja na kila walicho hitaji, na tumeongea na viongozi ambao wameturahisishia kila kitu ili tuweze kutekeleza majukumu yetu kwa urahisi na ukamilifu, yote haya yanatokana na utukufu wa Abulfadhil Abbasi (a.s)”.