Muhimu: Marjaa Dini mkuu anatoa pole kwa waathirika wa janga la Mosul na asema kua tukio hilo linatokana na ufisadi wa serikali.

Maoni katika picha
Marjaa Dini mkuu ametoa pole kwa waathirika wa mafuriko katika fukwe ya kitalii huko Mosul, iliyo poteza makumi ya raia, na ametoa wito wa kufanywa uchunguzi na kuwachukulia hatua wahusika, akasema kua tukio hili ni nehemu ya matunda ya ufisadi ulioenea katika taifa hili.

Ameyasema hayo katika khutuba ya pili ya swala ya Ijumaa ya leo (14 Rajabu 1440h) sawa na (22 Machi 2019m), iliyo swaliwa katika ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s) chini ya uimamu wa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i).

Ifuatayo ni sehemu ya khutuba hiyo:

Mabwana na mabibi tunaanza na kutoa pole kwa ndugu zetu huko Mosul na tunatuma rambirambi kwa wafiwa, pia tunatoa wito wa kufanyika uchunguzi na kubaini chanzo cha maji hayo kisha kumchukulia hatua za kisheria kila atakaye bainika kuhusika na janga hilo, hapa tutabainisha nukta mbili muhimu:

Kwanza: Lazima watu wawajibike yanapo tokea majanga kama haya kutoka katika wizara au idara husika, kwa kujiuzulu na kuwa chini ya kamati ya uchunguzi, inayo chunguza kama kuna athari za uzembe, na kuwa tayali kuwajibika kutokana na majibu ya uchunguzi, fahamu kuwa utaratibu huo ndio unaofatwa na nchi nyingi duniani, kufanya hivyo huonyesha kuwa kiongozi anawajali wananchi na yupo tayali kuwajibika, sio kufikiria uongozi tu na kufikiria maslahi binafsi pamoja na kungángánia madaraka.

Pili: Tukio hili linaonyesha upungufu mkubwa uliopo katika utendaji wa serikali, hii inatokana na kutowajibika kwa vyombo vinavyo husika, na hii ni miongoni mwa aina za ufisadi uliopo hapa nchini, kuna haja kubwa ya kuhakikisha sekta zote za serikali zinatimiza majukumu yao ipasavyo, mara nyingi uzembe kazini hutokana na kusameheana au rushwa, hii ni hatari sana ndio sababu kubwa ya kutokea matatizo katika sekta tofauti.

Tunataraji viongozi watatusikia na kuhisi upungufu pamoja na kuangalia namna ya kurekebisha upungufu huo, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu, aliokoe taifa letu na majanga pamoja na kila jambo baya, atulinde na majanga ya kimaumbile au ya kusababishwa, kwa utukufu wa Mtume Muhammad na Aali wake, na mwisho wa maombi yetu husema kila sifa njema anastahimi Mwenyezi Mungu Mola mlezi wa walimwengu na rehma na Amani ziwe juu ya Mtume Muhammad na Aali wake watakasifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: