Haya ndio maazimio ya wabunifu wa Iraq

Maoni katika picha
Kongamano na maonyesho ya pili ya wabunifu lililo fanywa chini ya kauli mbiu isemayo: (Karbala ni kitovu cha elimu na wanachuoni) lililo endeshwa na muungano wa wabunifu wa kiiraq chini ya ufadhili wa Atabatu Abbasiyya tukufu, wametoa mapendekezo na maazimio kadhaa waliyo yaona kuwa yanaweza kusaidia sekta ya ubunifu na kutatua baadhi ya changamoto, kwa mujibu wa maelezo ya mjumbe wa kamati kuu ya kongamano na maonyesho Dokta Khalid Ajamiy wakati akisoma maazimio, amesema kua:

Kutokana na tuliyo yaona katika siku tatu yametusaidia kutengeneza maazimio ambayo kama yakitekelezwa yatasaidia kufikia malengo ya kulitumikia taifa hili, tunatakiwa kunufaika na kundi la wasomi hawa katika sekta ya viwanda na uchumi wa Iraq.

Maazimio ni haya yafuatayo:

  • 1- Kuanzishwa kwa wizara na taasisi za serikali zenye uhusiano na ubunifu na zitakazo weza kufanyia kazi maazimio ya kongamano hili kwa faida ya wabunifu wa kiiraq na taifa kwa ujumla.
  • 2- Kuazimia kufanyika kwa kongamano na maonyesho ya tatu chini ya ufadhili wa Atabatu Abbasiyya tukufu, mara hii kwa hakika tumeridhishwa na ukarimu wa Ataba na tumekubaliana na uongozi wa Ataba kua; kongamano la awamu ya tatu liwe la kimataifa kwa kiwango cha asilimia %25 ya bunifu za kimataifa, huu ni ukarimu mkubwa ulio onyeshwa na uongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
  • 3- Tumekubaliana wabunifu wa viwanda wapewe fursa ya kuendeleza ubunifu wao katika viwanda vilivyo chini ya Atabatu Abbasiyya kwa kufanya kazi za kiuchumi zisizo haribu mazingira, chini ya makubaliano na muungano wa wabunifu wa kiiraq kupitia kamati maalum ya wabunifu.
  • 4- Atabatu Abbasiyya tukufu itachapisha kitabu kinacho elezea wabunifu wa kitaifa, na vitu walivyo buni pamoja na sambuli za ubunifu wao na uthibitisho kutoka mamlaka ya viwango na ubora pamoja na hati miliki zao, kutakua na aina ishirini za sambuli za viwandani.
  • 5- Umoja wa wabunifu usimamie kuanzishwa kwa wizara na taasisi za serikali kwa ajili ya kupanga bajeti ya kusaidia shughuli za ubunifu na tafiti za kielimu, kwa ajili ya ustawi wa taifa na maendeleo ya uchumi, azimio hili linatokana na mapendekezo ya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, na kujikita katika miradi itakayo saidia kuondoa tatizo la ajira na kukuza uchumi wa taifa.

Haya ndio maazimio kutoka katika kongamano na maonyesho yaliyo fanyika Karbala, na washindi walikua kumi na tano, wamepewa zawadi kutoka Ataba tukufu, kwa hakika tafiti zoto zilizo wasilishwa na wabunifu wote walio shiriki ni washindi, ni washindi kwa kuja Karbala, ni washindi kwa uzalendo wa taifa la Iraq, ni washindi kwa kuwepo ndani ya ukumbi huu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: