Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji mkono mmoja unalinda usalama na mwingine unatoa huduma katika maadhimisho ya alama za Mwenyezi Mungu.

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji, hakija jikita katika ulinzi wa Amani peke yake, bali kinashiriki katika shughuli zingine pia, ikiwa ni pamoja na kutoa huduma katika maadhimisho na maombolezo ya kuzaliwa na kufariki kwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s), na hutoa huduma kwa mazuwaru, mkono wao wa kutoa huduma umenyooka hadi kwa bibi Zainabu Sirya, na kuwahudumia watu waliokwenda kuomboleza kifo cha jemedari wa Karbala Hauraa Zainabu (a.s).

Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kimeweka maukibu Husseiniyya kwa ajili ya kutoa huduma karibu na malalo ya bibi Zainabu mtakasifu, katika maukibu hiyo wameshiriki watu wa idara ya ustawi wa jamii ambao wanatoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru watukufu.

Kiongozi mkuu (mushrifu) wa kikosi Ustadh Maitham Zaidiy alikuwepo huko na akafanya mazungumzo na mtandao wa Alkafeel, amesema kua: “Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kimepata utukufu wa kuhudhuria maombolezo ya bibi Zainabu (a.s) katika kumbukumbu ya kifo chake, kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kunaratiba kamili ya ugeni kutoka Ataba, na miongoni mwa ratiba hiyo ni maukibu hii, inayogawa chakula na vinywaji mbalimbali pamoja na kushiriki katika maukibu ya watu wa Karbala”.

Akaongeza kua: “Lengo kuu la kuja kwetu ni kuwahudumia mazuwaru wa Hauraa Zainabu (a.s) kama tulivyokua tukiwahudumia wageni wa Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya kuitikia wito wa Marjaa mkuu katika mji wa Najafu Ashrafu, na huu ni utukufu mkubwa kwetu, kuitikia wito wa Marjaa na kuadhimisha alama za Mwenyezi Mungu mtukufu”.

Kumbuka kua kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji hushiriki mara nyingi katika ziara mbalimbali zinazo fanywa kwenye Ataba tofauti ndani na nje ya Karbala, hufanya kazi mbili: kwanza kulinda Amani, na pili, kutoa huduma kwa mazuwaru
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: