Wakina Zainabu wanaomboleza kifo cha Aqiilah bani Hashim (a.s).

Maoni katika picha
Idara ya shule za Dini za Alkafeel za wasichana ambazo zipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya majlisi ya kuomboleza kifo cha kiigizo wao na muangaziaji wa njia yao bibi Zainabu (a.s), ndani ya Sardabu ya Imamu Mussa Alkadhim (a.s) katika Ataba tukufu, wameshiriki wanafunzi wengi wa viwango tofauti, ikiwa ni katika ratiba maalumu ya kuhuisha matukio ya Dini ya kuzaliwa na kufariki kwa Maimamu watakasifu, sambamba na kutoa mihadhara maalumu ya kuelezea historia ya Maasumina (a.s).

Kikao hiki kilikua na usomaji wa Quráni tukufu pamoja na muhadhara kuhusu mchango wa bibi Zainabu katika harakati ya kaka yake Imamu Hussein (a.s), pamoja na sifa kubwa aliyo kuwa nayo ya hijabu, kujihifadhi na elimu, na kusisitiza umuhimu wa kufuata mwenendo wake na kufanyia kazi kwa vitendo mafundisho yake.

Majlisi ikahitimishwa kwa kusomwa kaswida na ziara pamoja na kusoma duaáu Faraji, ya kuomba aje haraka msuluhishi wa umma Imamu Mahadi (a.f) pamoja na kuondoa wingu hili katika umma huu.

Kumbuka kua kuanzishwa kwa idara ya shule za Dini za wasichana Alkafeel kunatokana na kufanyia kazi maneno ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) yasemayo: (Kutafuta elimu ni faradhi kwa kila muislamu wa kiume na wa kike), na ikiwa ni miongoni mwa kazi kubwa zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kuanzisha vitengo bora vya elimu vinavyo jumuisha makundi yote ya kijamii wakiwemo wanawake, hii ni kutokana na umuhimu mkubwa walio nao katika jamii ya kiislamu na kuandaa kizazi chema.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: