Kukamilika kwa program za kongamano la mzaliwa wa Alkaaba (a.s).

Maoni katika picha
Kitivo cha utawala na uchumi katika chuo kikuu cha Basra kimekua mwenyeji wa hafla ya kufunga kongamano la mzaliwa wa Alkaaba, linalo fanywa kwa mwaka wa tatu, lililo ratibiwa na idara ya mahusiano na vyuo vikuu ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kushirikiana na uongozi wa chuo kikuu cha Basra, katika mnasaba wa kuzaliwa kwa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), na ikiwa ni sehemu ya mradi wa kijana wa Alkafeel mzalendo.

Hafla ya ufungaji wa kongamano ilikua na vipengele vingi, miongoni mwa vipengele hivyo ni:

Kwanza: Kikao cha majadiliano kilicho muhusisha mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu katika wilaya ya Zuberi kwenye mkoa wa Basra, Shekh Qassim Amuriy pamoja na wanafunzi wa kitivo cha utawala na uchumi wa chuo kikuu cha Basra, Shekh Amuriy amezungumzia nukta nyingi kuhusu mbora wa mawasii (a.s) miongo mwa nukta hizo ni:

  • - Hakika wanaomchukia Ali bun Abu Twalib (a.s) wanakua wametangaza vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake.
  • - Hakika Imamu Ali bun abu Twalib (a.s) haukuongezeka utukufu wake kwa kuzaliwa ndani ya Alkaaba, bali Alkaaba ndio iliongezeka utukufu kwa yeye kuzaliwa humo.
  • - Hatuwezi kuhesabu utukufu wake katika vitabu, waandishi wa vitabu kila sehemu ya dunia bado wanajifunza maneno ya Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s) katika nahaju balagha.

Baada yake ukafunguliwa mlango wa majadiliano na wanafunzi na Shekh Amuriy akawa anajibu maswali kuhusu mada aliyo toa na mengineyo na kutoa ufafanuzi zaidi.

Pili: Kutolewa muhadhara wa kitabibu kuhusu njia za kutoa huduma ya kwanza kwa mgonjwa, uliotolewa na mkufunzi kutoka idara ya utowaji wa huduma ya kwanza kwa wagonjwa katika Atabatu Abbasiyya tukufu, amezungumzia namna ya kupambana na matatizo ya mafuriko, kumeza ulimi na mengineyo, mambo ambayo yanaweza kumtokea mtu yeyote katika maisha yake ya kila siku.

Tatu: kutolewa kwa muhadhara kuhusu Quráni, uliokua na kichwa cha habari kisemacho: (Nafahaatu Qurániyya), uliotolewa na msomaji wa Atabatu Abbasiyya tukufu bwana Muslim Shabakiy, amefafanua umuhimu wa Quráni tukufu katika maisha ya kila siku na njia za kuitafakari na kufahamu maana yake na kuifanyia kazi.

Kwa upande wao; wanafunzi wa utawala na uchumi katika chuo kikuu cha Basra wameonyesha kufurahishwa na kongamano hili, na wamesifu mihadhara waliyo pewa na kusema kuwa ilikua mizuri, wakaeleza kuwa jambo hili sio jipya kwa Atabatu Abbasiyya tukufu, kwani daima imekua ikijenga uwelewa wa mambo mbalimbali kwa wanafunzi wa vyuo vikuu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: