Atabatu Abbasiyya tukufu yahitimisha majlisi ya kuomboleza katika malalo ya bibi Zainabu (a.s).

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imehitimisha majlisi ya kuomboleza iliyo dumu siku mbili, ambayo hufanywa kila mwaka katika malalo ya bibi Zainabu (a.s), mzungumzaji katika majlisi hizo alikua ni Shekh Abduswahibu Twaaiy na waimbaji wawili, bwana Haidari Atwaari na Hussein Akili, majlisi ilikua na mahudhurio makubwa kutoka kwa mazuwaru waliokuja kuhuisha ahadi na utiifu wao kwa Aqiilah bani Hashim (a.s).

Ratiba ya majlisi ilikua inaanza baada ya swala ya Isha, na ilikua inafunguliwa kwa Quráni tukufu, kisha unafuata muhadhara wa Shekh Abduswahibu Twaaiy ambaye ni kiongozi wa idara ya wahadhiri katika Atabatu Abbasiyya tukufu, alimzungumzia bibi huyu mtukufu aliye rithi matatizo ya mama yake, akaishi katika shida na machungu hadi kufariki kwake, akataja baadhi ya matatizo akiyo pitia katika maisha yake, na nafasi yake katika kuendeleza mapinduzi ya kaka yake, baada yake alikua anapanda jukwaa mwimbaji wa kaswida za Husseiniyya bwana Haidari Atwari na Hussein Akili, na majlisi inahitimishwa kwa kuwaombea dua umma wa kiislamu na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) koto duniani.

Shekh Abduswahibu Twaaiy kiongozi wa idara ya wahadhiri katika Atabatu Abbasiyya amesema kua: “Kwa baraka za bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) tumefanya majlisi za kuomboleza katika haram ya bibi Zainabu (a.s), kutoa huduma hii ni taufiki kubwa, ukizingatia kua tumekuja kwa jina la mwezi wa familia (a.s), chini ya maelekezo ya viongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu ya kutaka majlisi hii iendelee kufanywa kila mwaka, kuna fikra kuwa majlisi zifanywe ndani ya haram ya Zainabu katika kila tukio la kidini, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awawezeshe watumshi wote wa Abulfadhil Abbasi (a.s) waliotoa kila aina ya huduma katika ugeni huu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: