Kituo cha Swidiiqah Twahirah (a.s) kinafanya mashindano ya wasichana ya kuhifadhi Duaául-Ahdi.

Maoni katika picha
Kutokana na maneno ya Imamu Swadiq (a.s) yasemayo: (Atakaye muomba Mwenyezi Mungu asubuhi arubaini kwa Duaául-Ahdi atakua miongoni mwa answaari wa Qaaimu wetu, na akifa kabla yake, Mwenyezi Mungu atamtoa katika kaburi lake na atampa kwa kila neno thawabu elfu moja na kumfutia dhambi elfu moja), kituo cha Sweidiiqah Twahirah (a.s) chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kinaendesha shindano la kuhifadhi Duaául-Ahdi, iliyo pokewa na Imamu Swadiq (a.s) kwa wanawake wa rika zote, kwa ajili ya kushajihisha kuhifadhiwa dua hiyo na kubainisha umuhimu na utukufu wake.

Kituo kimetoa wito kwa kila anayetaka kushiriki afike katika ofisi za kituo hicho zilizopo katika mtaa wa Mulhaq jirani na jengo la Swahibu Zamaan saa tatu asubuhi siku ya Jumamosi (7 Shabani 1440h) sawa na (13/04/2019m).

Kituo kimeandaa zawadi za washindi kumi za mali na tabaruku kutoka katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: