(Na katika hayo washindane wenye kushindana) watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wameifanya aya hii tukufu kuwa kauli mbiu yao, wanashindana wao kwa wao katika kutoa huduma kwa mazuwaru wa kubba za dhahabu katika mji mtukufu wa Karbala, safari hii wamepanua huduma zao na kwenda kumhudumia dada yake jemedari wa Karbala Hauraa Zainabu (a.s) na mazuwaru wake.
Kiongozi wa ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu na rais wa kitengo cha kusimamia haram bwana Hassan Hilali amesema kua: “Kwa Baraka za tunaye mtumikia Abulfadhil Abbasi (a.s) na mazuwaru wake, tumegawa mamia ya sahani za chakula kwa watumishi wa dada yake Hauraa Zainabu (a.s) na mazuwaru wake, tumegawa mamia ya chakula kupitia maukibu ya utumishi tuliyo iweka karibu na haram tukufu, tulianza kugawa chakula kabla ya siku ya tukio na baada yake”.
Wahudumu wameonyesha furaha yao kwa kupata nafasi ya kutoa huduma hii, wakasema kua ni neema kubwa waliyo pewa na Mwenyezi Mungu, ya kumtumikia Hauraa Zainabu (a.s) na mazuwaru wake.