Jopo la wahandisi wa kiiraq: Miradi inayofaywa na Atabatu Abbasiyya ni fahari kwa wahandisi wa Iraq.

Maoni katika picha
Jopo la wahandisi wa kiiraq katika tawi la Karbala kwa kushirikiana na kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu, wamefanya nadwa chini ya anuani isemayo: (Haki za wahandisi wa Iraq), nadwa hii inakusudia kuongeza uwezo wa wahandisi na kubadilishana uzowefu baina ya Atabatu Abbasiyya tukufu na jopo la wahandisi wa kiiraq, kwa ajili ya kuboresha mazingira ya wahandisi hapa nchini, nadwa imehudhuriwa na marais wa matawi kutoka kwenye mikoa nane ambayo ni: (Basra, Misaan, Muthanna,Qadisiyya, Baabil, Waasid, Swalahu-Dini, Diyala), pamoja na wawakilishi wa kituo kikuu cha wahandisi.

Nadwa imejadili mazingira ya wahandisi na mahitaji muhimu yatakayo wasilishwa serikalini na kwenye taasisi maalumu, sambamba na kudai haki za wahandisi kama zinavyo daiwa na jamii ya wahandisi wa Iraq.

Baada ya hapo jopo la wahandisi wa kiiraq pamoja na marais wa matawi walitembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na wakapewa maelezo kwa ufupi kuhusu miradi hiyo, na wakapewa nafasi ya kuuliza maswali na kupewa ufafanuzi zaidi, mwishoni mwa matembezi hayo wageni walionyesha kufurahishwa sana na miradi waliyo tembelea, wakasema kua inaonyesha wazi kuwepo kwa utawala bora na utendaji makini, wakasisitiza kua; miradi inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu ni fahari kwa wahandisi wote wa Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: