Atabatu Abbasiyya tukufu yapokea wanafunzi na walimu kutoka chuo cha ufundi cha Karbala.

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu katika ratiba yake ya kupokea ugeni wa wanafunzi wa vyuo na wakufunzi wao, inayo tekelezwa na idara ya mahusiano na vyuo vikuu chini ya kitengo cha uhusiano, imepokea wanafunzi na walimu wa chuo cha ufundi cha Karbala, ambacho kipo chini ya chuo kikuu cha Furat Ausat.

Ratiba ya ziara hii ilikua na vipengele vingi, miongi mwa vipengele hivyo ni:

Kwanza: Kutembelea malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), ibada hiyo ilihitimishwa kwa kupiga picha ya pamoja, iliyo pigwa na mmoja wa watumishi wa Ataba mbili tukufu, kisha wakaenda kuswali sunna ya ziyara na kusoma dua.

Pili: Kutembelea korido za ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuangalia miradi inayo fanywa kwa sasa, ambayo ni uwekaji wa marumaru katika haram pamoja na kupewa maelezo ya kazi zilizo kamilika, kupitia watumishi wawili walio fuatana na wageni, halafu wakaenda katika kitengo cha zawadi na nadhiri cha Atabatu Abbasiyya tukufu, wakasikiliza maelezo na kuangalia utendaji wa kitengo hicho, namna kinavyo pokea zawadi na mambo mengine.

Tatu: Walifanya mazungumzo na Sayyid Muhammad Mussawi kutoka kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu, wakazungumzia mambo mengi yanayo husu wanafunzi na walimu, pakasemwa kua kila mtu anavyo zidi kuwa na elimu ndio anavyo zidi kupata mitihani na kuwa karibu na Mwenyezi Mungu mtukufu.

Kisha wakapewa karatasi ili kila mmoja aandike maswali au maoni yake kuhusu nadwa au kitu kingine chochote, Sayyid Mussawi akajibu maswali na kufafanua Zaidi pale alipo takiwa kufafanua, mwisho wa ziara hii wageni wameishukuru sana Atabatu Abbasiyya tukufu na wafanyakazi wote kwa mapokezi mazuri na faida kubwa waliyo pata katika ziara yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: