Kwa ushiriki wa zaidi ya watu (60): Ufungaji wa semina za Rasulul Aádham na Sayyidul Maa za Quráni.

Maoni katika picha
Katika muendelezo wa semina za Quráni zinazo endeshwa na Maahadi ya Quráni tukufu katika Atabatu Abbasiyya, kuhusu hukumu za tajwidi, sauti na naghma. Idara ya usomaji na kuandaa wasomaji imefunga semina mbili za Quráni, semina ya Rasulul Aádham (s.a.w.w) na Sayyidul Maa (a.s), kwa usomaji wa mahadhi ya kiiraq na kimisri, hayo ni mahadhi yenye unyenyekevu na huzuni wakati wa usomaji, riwa tukufu zinatutaka tusome Quráni kwa unyenyekevu na huzuni, ikiwemo iliyo pokelewa na Imamu Abu Abdillahi Swadiq (a.s) isemayo: (Hakika Quráni imeteremka kwa huzuni isomeni kwa huzuni).

Semina mbili hizo zilikua na washiriki (60) kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala, chini ya wakufunzi mahiri walio wezesha kupatikana kwa idadi hiyo ya wanafunzi walio hitimu usomaji wa Quráni kwa mahadhi mbili.

Masomo yaliyo fundishwa ni, hukumu za usomaji, sauti, naghma, maqamaat asilia na zisizo asilia, sambamba na mahadhi ya kiiraq na kimisri, wasimamizi wa semina walikua ni, Ustadh Alaa Dini Hamud na Sayyid Haidari Jalukhaan.

Mkuu wa Maahadi ya Quráni tukufu Shekh Jawadi Naswirawi akizungumza katika hafla ya ufungaji ameeleza utukufu wa Quráni na nafasi ya mtu anaye ifundisha na kujifundisha, akaonyesha matarajio makubwa kwa wahitimu wa semina hizi waende wakawafundishe watu wengine katika miji yao.

Kwa upande wa wahitimu katika ujumbe waliotoa kwenye hafla hiyo, wameishukuru sana Atabatu Abbasiyya tukufu na Maahadi ya Quráni pamoja na walimu wake, kwa kazi kubwa waliyo fanya ndani ya miaka miwili kwa kuwafundisha usomaji wa kitabu cha Mwenyezi Mungu kitukufu.

Kumbuka kua mafunzo haya ni sehemu ya semina nyingi zinazo tolewa na idara ya usomaji kwa lengo la kuandaa wasomaji bora watakao tumikia uwanja wa Quráni hapa Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: