Idara ya wahadhiri wa kike inaendelea na ratiba ya kuwapongeza wasichana wanaofikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria.

Maoni katika picha
Katika kutekeleza ahadi waliyo jiwekea, ya kuzifikia shule nyingi Zaidi katika mkoa mtukufu wa Karbala, na kufuatia kauli mbiu wanayo tumia isemayo (Kwa nuru ya Zaharaa tumeongoka), viongozi wa idara ya wahadhiri wa kike wanaendelea na ratiba yao ya kiroho na kimaadili, kuwapongeza wasichana wanaotimiza umri wa kuwajibikiwa na sharia, ratiba iliyo anza kutekelezwa katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwa bibi Zaharaa (a.s), hii inatokana na namna Atabatu Abbasiyya tukufu inavyotilia umuhimu swala la kuwaelemisha mabinti umuhimu wa umri huo, na kutambua majukumu yao kisheria, ili kuwafanya watekeleze sharia za Mwenyezi Mungu ambazo huimarisha uhusiano kati ya mja na Mola wake, kama vile swala ni ibada inayo mzuwia mja kufanya maovu na uchafu, na kuhusu uhusiano wake na jamii upo katika hijabu.

Makamo kiongozi mkuu wa idara ya wahadhiri wa kike Ustadhat Taghridi Abdulkhaliq Tamimi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Pamoja na kua huu ni mwaka wa kwanza kufanya ratiba hii, imepata mwitikio mkubwa, na tumeweza kufikia shule nyingi hasa zilizopo vijijini ambazo zilikua hazijashuhudia hafla za aina hii, imekua fursa ya kufanya hafla na kuwapongeza wasichana wanaofikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria, na kuangalia mazingira ya shule hizo pamoja na kufungua mlango wa mawasiliano kati ya shule hizo na ofisi yetu, kwa ajili ya kuendelea kushirikiana katika harakati zinazo fanywa na shule hizo au na Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akaendelea kusema: “Program tuliyo fanya inavipengele vingi, miongoni mwa vipengele hivyo ni:

  • - Muhadhara kuhusu hijabu na umuhimu wake kwa msichana.
  • - Usomaji sahihi wa surat Fat-ha pamoja na vipande vya tafsiri za baadhi ya aya sambamba na shuhuda kuhusu umuhimu wa hijabu.
  • - Masomo kuhusu historia ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s) na kuangalia hadithi zao pamoja na kuzilinganisha na mazingira halisi ya sasa.
  • - Masomo ya kifiqhi na kiaqida yanayo endana na umri wao.
  • - Vipindi vya mapumziko.
  • - Kuswali kwa jamaa.

Wamepewa nguo za kuswalia na zawadi za tabaruku kutoka kwa Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na vipeperushi vinavyo himiza uvaaji wa hijabu na kujifundisha swala na ibada zingine kwa undani”.

Idara za shule zimepongeza sana jambo hili linalo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, la kuendesha program inayo onyesha kukijali kizazi cha sasa hasa wasichana, kwa kuwapa mafundisho yanayo endana na umri wao.

Kumbuka kua umri wa kuwajibikiwa na sharia ni utamaduni uliopo katika uislamu na Atabatu Abbasiyya inautilia mkazo, na kuufanya kuwa msingi wa kutoa malezi ya kimaadili katika jamii, hakika umri huo ni msingi wa kumtoa kijana katika hatari na kumuweka mahala salama.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: