Semina hiyo imefanyika ndani ya ukumbi mkuu wa sekondari ya Ameed chini ya ukufunzi wa Mhandisi Muhammad Mustwafa na Bilali Jabbari, wamefafanua namna ya kutumia vifaa vya zimamoto katika mazingira hatari, wakaelezea mambo kadhaa ya muhimu kuzingatiwa, miongoni mwa mambo hayo ni:
- 1- Kifaa cha otumatik na cha kutumia mkono na uwezo wake katika kuzima moto na kubunguza madhara yake.
- 2- (Vifaa vya nyumbani) ni sababu kubwa ya kutokea moto katika nyumba, lazima kuwa makini na kuchukua tahadhari za kiusalama katika matumizi.
- 3- Kuainisha baadhi ya vifaa vinavyo sambaza moto haraka na namna ya uwakaji wake.
Halafu ukafuata usomaji kwa vitendo namna ya kuzima moto kwa kufuata kanuni za uzimaji, wanasemina wote wameshiriki katika zowezi hilo.
Wanafunzi wa sekondari ya Ameed wameishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia jopo la wakufunzi wa usalama kwa kuwapa semina hii, wakasema kuwa inafaida kubwa kijamii, kielimu na kifamilia, inalenga kuimarisha uthubutu wa kutoa huduma za awali na kupambana na majanga ya moto na mengineyo, jambo ambalo hupunguza ukubwa wa hasara za mali na nafsi.
Tunapenda kukufahamisha kua Atabatu Abbasiyya tukufu huendesha nadwa, semina na mihadhara mbalimbali kuhuru utowaji wa huduma ya kwanza na uwokozi, pamoja na kupambana haraka na matukio ya moto, kwenye miji tofauti, kwa kutumia wataalamu walio bobea katika fani hizo.