Dokta Saidi Hakim Kaadhim rais wa jopo la majaji wa shindano la nne la kitaifa kuhusu utowaji wa khutuba, lililo anza asubuhi ya Alkhamisi (20 Rajabu 1440h) sawa na (28 Machi 2019m) amesema kua: “Hongera kwa kila anaepongeza ushindi wa jeshi na raia wake katika ardhi takatifu, na maneno yake yakaungana na bwana wa waaminifu”.
Akabainisha kua: Katika asubuhi hii, mapenzi ya taifa na Ahlulbait (a.s) yamekutana, tupo chini ya hema lao kwa ajili ya kutuliza nafsi zetu na kupata Amani ya nyoyo zetu, hongera kwa kila aliye tembea masafa kwa ajili ya kuja hapa, na leo yupo mbele ya haram ya bwana wa utukufu na uwaminifu (a.s), amepata makusudio yake ya kukaa chini ya kivuli cha mti wenye mizizi madhubuti (mirefu) na matawi yake ni utukufu, uaminifu na utakatifu, karibu sana kwa kila aliyekusudia kufasiri ujumbe wake kwa Imani na kuongeza taqwa, huku akijitahidi kufasiri maneno yake na kuonyesha mapenzi ya taifa lake, kwa kuwa kupenda taifa ni katika Imani, hongara kwa kila aliyekuja kupongeza ushindi wa taifa lake dhidi ya maadui wa Daesh, na kuunganisha maneno yake mbele ya bwana wa watekelezaji.
Akaongeza kua: “Kila mkutano na katika kila mwaka tunasikia maneno matamu kuhusu taifa, wamekuja kusema maneno yao katika jengo lako kwa sababu utukufu wako ni Zaidi ya taifa na unasifika kwa uwaminifu, wamekuja mbele yako ili utie Baraka na kukubalika maneno yao, hawajaona mwingine zaidi yako, ndio maana wamekusanyika ndani ya haram yako, ili maneno yao yazunguke mbele yako na katika malalo ya bwana wa mashahidi (a.s), ili wapate ladha ya maisha, hakuna katika wao ispokua waliofaulu, sauti zao zibarikiwe na waliohudhuria pia wabarikiwe na wapate thawabu”.
Akamaliza kwa kusema: “Shukrani ziwaendee watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu ambayo imefanya kila iwezalo kuhakikisha taifa letu linakuwa katika kheri ya elimu na maarifa, na liwe taa iangazayo na kustarehesha, tunashukuru sana saiti zinazo pazwa za kuipenda Iraq, sauti zinazo ondoa uchovu wa safari na kufuta vumbi la huzuni kwa taifa letu, maneno yao yatapelekea hija yenye kukubaliwa na juhudi zenye kushukuriwa katika uwanja wa mkarimu na mtowaji mtukufu”.