Maandalizi ya maonyesho ya vitabu ya kimataifa hapa Karbala yanaendelea.

Maoni katika picha
Kutokana na kukaribia ufunguzi wa maonyesho ya vitabu, mafundi na wahandisi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wanafanya ujenzi na matengenezo ya eneo yatakapo fanyikia maonyesho hayo ya kimataifa hapa Karbala, yatakayo anza (28 Rajabu) hadi (8 Shabani) katika eneo la uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, maonyesho haya ni miongoni mwa vipengele muhimu zaidi vya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada ya kumi na tano.

Wanafanya kazi ya kugawa vizimba maalumu kwa kila tawi au taasisi itakayo shiriki katika maonyesho sambamba na kukadiria ukubwa wa kila kizimba na kuweka shelfu zitakazo tumika kuonyeshea vitabu.

Kazi hii ilitanguliwa na kazi ya kuosha eneo hilo, iliyo fanywa na watumishi wa Ataba mbili tukufu, sambamba na kufanya matengenezo ya taa, feni na mfumo wa zimamoto, pia eneo hilo limefungwa kwa matumizi mengine ya mazuwaru hadi utakapo fanyika ufunguzi wa maonyesho ya vitabu, kazi hii itaendelea kufanywa kila siku hadi karibu na muda wa kuanza maonesho.

Fahamu kua maonyesho ya vitabu ya kimataifa ni miongoni mwa vipengele muhimu vya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada katika kila mwaka, huandaliwa na kusimamiwa na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, daima Ataba mbili tukufu zimekua zikitilia umuhimu mkubwa maonyesho haya, hushiriki makumi ya taasisi za usambazaji wa vitabu kutoka ndani na nje ya Iraq, ambao huonyesha vitabu vya aina mbalimbali na vilivyo andikwa kwa lugha zaidi ya moja.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: