Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i), amesifu ushindi aliopata mtafiti na mtumishi wa kituo cha faharasi na kupangilia maalumaat chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Ataba tukufu, Ustadh Bahaau Twalibu Abdu amekuwa mshindi katika kongamano na maonyesho ya mwaka wa ishirini na tano yanayo simamiwa na jumuwia ya Maktaba tawi la nchi za kiarabu, ambako walialikwa na idara ya utamaduni na utalii ya Imaraat, na kongamano likafanywa chini ya kauli mbiu isemayo: (Intanet ya vitu: Mustakbali wa jamii ya Intanet zenye mfungamano), na kupata tuzo ya mtafiti bora, akiwa miongoni mwa makumi ya watafiti wa kiarabu, tozo hiyo ameipata kutokana na utafiti wake usemao: (Zana za kufuatilia –Beacon- utendaji wa Maktaba).
Mheshimiwa amesisitiza kua –sawa awe mtafiti au mtu yeyote anayefanya kazi katika Atabatu Abbasiyya tukufu- anapo fanya juhudi za ziada katika kufanya utafiti, tutampongeza na kubainisha uwezo wa mfanyakazi wa Ataba tukufu, akasisitiza kua, Atabatu Abbasiyya na viongozi wake watakua msaada mkubwa katika mambo hayo.
Kwa upande wake Ustadh Bahaau Twalibu Abdu, tuzo yake ameitoa zawadi kwa bosi wake anaye mtumikia Abulfadhil Abbasi (a.s), akizingatia kuwa yeye ndio mwaalimu wake wa kwanza, na ametoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria kwa msaada wake endelevu katika sekta zote za Atabatu Abbasiyya tukufu.