Maoni katika picha
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi wa Ataba tukufu pamoja na wazazi wa wanafunzi, na imefunguliwa kwa Quráni tukufu pamoja na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukaimbwa wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu (Lahnul-Iba).
Ukafuata ujumbe wa Ataba tukufu ulio wasilishwa na mjumbe wa kamati kuu ya uongozi Dokta Abbasi Mussawi, akasema kua: “Hakika yakini hii katika kufuata njia sahihi na nyayo za waja wema waliofuata uongofu wa Mitume (a.s), ni furaha iliyoje kwetu tunapo hisi kuwa tumeweka miguu yetu katika nyayo zao na kufuata mwenendo wao mtukufu, hususan siku ya leo ambayo tunawapongeza mabindi zetu watukufu kwa kufikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria na kuwa askari wa bibi Zaharaa (a.s)”.
Akaongeza kua: “Mabinti (390) wamevaa nguo nyeupe zinazo ashiria weupe wa kurasa zao hapa duniani, zitakazo jazwa mambo mema kwa baraka ya baba zao na mama zao pamoja na juhudi za walimu wao yanayo mfurahisha kiongozi wetu (a.s), enyi mabinti wa Batuli shikamaneni na mwenendo mwema utakao wavusha salama”.
Akabainisha kua: “Hafla hii sio kutoa pongezi kwa mabinti peke yake, bali ni ushahidi kwetu pia wa mabinti walio ingia katika utukufu wa Mwenyezi Mungu, na kushuhudia jambo jema huwafanya malaika waandike mambo mema, mnatakiwa kumtii Mwenyezi Mungu na wazazi wenu pamoja na kushikamana na ibada, na mfuate mwenendo wa wakina mama wema kama vile bibi Zaharaa (a.s), mkifanya hivyo mtafaulu”.
Akaongeza kua: Enyi mabinti zangu wazuri jipambeni na uchamungu na maadili mema sio utembezi na uchafu, ndugu zangu waumini, ndugu zandu wazazi.. hawa mabinti ni amana ya Mwenyezi Mungu kwenu watunzeni vizuri, na nyie ni waaminifu wa kulinda amana.
Ndugu zangu walimu Mwenyezi Mungu abariki juhudi zenu, nyie ni mkono wa pili katika kulinda amana hii, katika kuwalea mabinti hawa, nawashukuru sana kwa kufanya hafla hii kwa ajili ya mabinti hawa watukufu nawatakia taufiq daiama.
Hafla ilikua na mambo mbalimbali yaliyo fanywa na mabinti, waliimba utenzi usemao: (kuwajibikiwa kwangu kunatoka kwa Mola wangu), kisha wakakariri kiapo kitukufu (kiapo cha kuwajibikiwa na sharia), na wakafanya igizo kuhusu hijabu, halafu wakapewa zawadi ya vitu kama vile (hijabu, mswala, turba, tasbihi na Quráni) vitu wanavyo takiwa kuvitumia katika umri huu wa kuwajibikiwa na sharia.
Mfano wa hafla kama hii imefanywa jioni kwa ajili ya wavulana, mjumbe wa kamati kuu ya uongozi ya Atabatu Abbasiyya Dokta Abbasi Mussawi alipata nafasi ya kuongea, akasema kua: “Hakika leo tunawapongeza vijana wetu na kuwavusha katika uchamungu na kufuata nyao za watu wa nyumba ya Mtume (a.s)”.
Akafafanua kua: “Vijana (180) waliovaa nguo nyeupe zinazo ashiria weupe wa kurasa zao zinazo takiwa zijazwe mambo ya kheri, -Insha-Allah- chini ya usimamizi wa wazazi na walimu wao, wanatakiwa kufanya mambo yatakayo mridhisha Imamu (a.s)”.
Baada yake ukafuata ujumbe elekezi kutoka kwa Sayyid Muhammad Mussawi mtumishi wa kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kisha wanafunzi wakafanya maigizo mbalimbali, kuhusu Imamu Mahadi (a.f) na linguine kuhusu kudumu katika kumpenda Imamu Hussein (a.s) pamoja na igizo kuhusu uzembe wa wazazi katika kuwasaidia watoto wao kwenye masomo..
Mwisho wa hafla wanafunzi hao wakapewa zawadi baada ya kukariri kiapo cha kuwajibikiwa na sheria.