Atabatu Kadhimiyya imepandisha bendera za huzuni kama tangazo la kuomboleza kifo cha Imamu Mussa Alkadhim (a.s).

Maoni katika picha
Kwa mara nyingine wapenzi wa Ahlulbait (a.s) wanahuisha maombolezo yao, kwa kumkumbuka Imamu wao Kaadhimul-Ghaidh (a.s), na mateso aliyofanyiwa na watawala wa bani Abbasi akiwa gerezani, wamesimama kuitikia wito wa kiongozi wao aliye uwawa kwa sumu, mlango wa wenye haja Imamu Mussa bun Jafari Alkaadhim (a.s), huku wakiwa wamepandisha bendera ya huzuni na maombolezo, ukumbi wa haram tukufu ya Kadhimiyya jioni ya Ijumaa (21 Rajabu 1440h) sawa na (29 Maji 2019m) umeshuhudia tukio la kubadilisha bendera za kubba mbili za Maimamu wawili Aljawadaini (a.s), zimepandishwa bendera nyeusi zinazo ashiria huzuni na msiba, katika mkusanyiko mkubwa wa watu, ulio hudhuriwa pia na katibu mkuu wa Atabatu Kadhimiyya Dokta Jamali Abdurasuul Dabaagh pamoja na wajumbe wa kamati kuu ya uongozi, na mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Shekh Hussein Aali Yaasin, na kundi kubwa la masayyid na mashekh watukufu, sambamba na wawakilishi wa Ataba na mazaru, bila kuwasahau viongozi mbalimbali na mazuwaru wa Maimamu wawili Aljawadaini (a.s).

Hafla ilifunguliwa kwa Quráni tukufu iliyo somwa na msomaji wa Ataba tukufu Dokta Raafií Aláamiriy, baada yake zikafuata mawakibu za Kadhimiyya zikafanya maombolezo ya utamaduni wao wakiwa wamebeba bendera za utiifu, halafu ukafuata ujumbe wa Atabatu Kaadhimiyya tukufu ulio wasilishwa na katibu wake mkuu, amesema kua: “Nikawaida ya madhalimu wa kila zama kuwadhalilisha mawalii wa Mwenyezi Mungu walio tukuzwa na Mwenyezi Mungu na kupewa madaraka ya kuongoza umma, wameamua kuweka pingamizi katika safari ya mwanaadamu kwa ajili ya kufuata matamanio yao, kwa kupanua utawala wao na kutesa waja wema huku wakiwa wamezama katika mambo ya haram, miongoni mwa zama za watawala waovu ni zama ya Imamu Kaadhim (a.s) aliye nyanyaswa na Twaghuti wa zama zake, wakati Imamu (a.s) alipo wathibitishia walimwengu uwovu wa watawala wa zama zake na kutofuata kwao mwenendo sahihi wa kiislamu, waliamua kumuua kwa sumu, historia imekataa kumsaham Imamu hadi mji umeitwa kwa jina lake na utukufu wake utazungumzwa milele, na historia imemfuta adui wake na mji aliokua akidai kuwa ni mji wake umemkataa hata sehemu ya kaburi lake imepotea”.

Akaongeza kua: “Hakika katika mwenendo wa Imamu (a.s) na jihadi yake kuna masomo mengi, yatupasa kunufaika nayo, katika mwenendo wake (a.s) tunajifundisha kuzuwia hasira na kuwa na subira tunapo patwa na matatizo, na umuhimu wa kuamrisha mema na kukataza mabaya pamoja na kurekebisha umma, na kusaidia aliye dhulumiwa na kuto muunga mkono dhalimu”.

Kisha ukafuata ujumbe kuhusu mradi wa tabligh katika hauza tukufu, ulio wasilishwa na mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu katika mji wa Kaadhimiyya Mheshimiwa Shekh Hussein Aali Yaasin, akaanza kwa kutoa pole kwa Maimamu wawili Jawadaini (a.s) na Imamu hujjat (a.f) kwa niaba ya wapiganaji waliopo katika uwanja wa mapambano na kwaniaba ya mashahidi na majeruhi pamoja na familia zao, akabainisha kua: “Jukumu la Mubaligh ni kulingania Dini asilia na kufundisha kitabu na sunna zilizo thibiti, na mema ya Mtume (s.a.w.w) pamoja na Maimamu watakasifu (a.s), kuwapa watu mawaidha na kuwaelekeza mambo mema ili wazidi kumwamini Mwenyezi Mungu mtukufu, na mubaligh anatakiwa aishi vizuri na watu wote hadi wa Dini tofauti, hatakiwi kutumia mimbari kama sehemu ya kutangaza maoni yake binafsi na kuleta fitna na mifarakano, yeyote atakaetumia mimbari kwa maslahi binafsi waumini hawapaswi kumtii”..

Akaongeza kua: “Huu ndio ujumbe wa mradi wa tabligh, tabligh ni kuwatumikia watu wote, kwa utukufu wa hauza, walimu, wanafunzi kama nilivyo zowea kuwakumbusha misingi ya utukufu wa uislamu, na kujibu mambo tofauti ya kisheria na kusikiliza shida za watu kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu mtukufu chini ya usimamizi wa Marajaiyya tukufu, nikisaidiwa na idara za Ataba tukufu, bila kuusahau uongozi mkuu wa Atabatu Kaadhimiyya takatifu, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu akubali ibada zenu na ziara yenu pamoja na vilio vyenu kutokana na msiba huu mkubwa wa Aali Muhammad (a.s).

Baada ya kumaliza kuongea bengera za kubba mbili zikashushwa na kupandishwa bendera nyeusi.

Kisha Shekh Saidi Maátiiq akasoma kaswida zilizo amsha hisia za huzuni kwa wahudhuriaji na kuhitimishwa kwa kaswida na mashairi yaliyo somwa na Ammaar Kinani ya kuomboleza msiba huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: