Askari (500) wa kikosi cha Abbasi na ndege zisizokua na rubani wanajitolea kuimarisha ulinzi katika ziara ya Imamu Alkaadhim (a.s).

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kimejitolea mamia ya askari wake, kwenda kusaidia ukaguzi kwenye barabara zinazo ingia katika mji wa Kaadhimiyya tukufu katika kipindi hiki cha kumbukumbu ya kifo cha Imamu Mussa Alkaadhim (a.s), jambo hili lipo katika mkakati wa kikosi cha Abbasi (a.s) la kuimarisha ulinzi katika ziara hii.

Vilevile wanatumia ndege zisizokua na rubani kulinda anga la mji wa Kadhimiyya unaoshuhudia mamilioni ya mazuwaru kwa sasa kutoka sehemu tofauti ndani na nje ya Iraq.

Kiongozi mkuu wa kikosi cha Abbasi Ustadh Maitham Zaidi amesema kua: “Tumeandaa askari wa kujitolea (500) kwa ajili ya kusaidia wanaeshi kazi ya ukaguzi, na kulinda mazuwaru wanao miminika kwa wingi katika mji mtukufu wa Kadhimiyya kuja kuomboleza kifo cha Imamu Mussa Alkaadhim (a.s)”.

Pia wanatumia ndege zisizokua na rubani katika kulinda anga la mji wa Kadhimiyya kutokana na tishio lolote la kuwadhuru mazuwaru na kutishia usalama wao.

Akasema: “Mambo yote yanafanywa kwa kuwasiliana na askari wa muungano kikosi cha pili”.

Fahamu kua kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kabla ya siku chache kulishiriki katika kuhuisha kumbukumbu ya kuomboleza kifo cha bibi Zainabu (a.s) nchini Sirya, kupitia msafara mkubwa uliotumwa na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: