Kituo cha kurekebisha nakala kale kinafanya warsha katika chuo kikuu cha Baabil.

Maoni katika picha
Miongoni mwa vituo hai vya maktaba na Darul Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya ni kituo cha kurekebisha nakala kale, ambacho kimechukua jukumu la kuchangia katika uhuishaji wa nakala kale na urithi wa elimu ya uislamu, kimepiga hatua kubwa katika sekta hiyo, kutokana na uwezo mkubwa walio nao pamoja na vifaa vya kisasa.

Atabatu Abbasiyya tukufu inatilia umuhimu kueneza elimu hiyo katika taasisi zingine zinazo fanana nayo pamoja na taasisi za kisekula, kituo kimeandaa warsha katika chuo kikuu cha Baabil, kwenye warsha hiyo wamezungumzia pande mbili (nadhariyya na vitendo), wametoa ufafanuzi kuhusu nakala kale na aina zake, pamoja na njia za utunzwaji wake, pia wamefanya kwa vitendo kazi ya kurekebisha baadhi ya karatasi zilizoharibika.

Program hii imepata mwitikio mkubwa, imehudhuriwa na wanafunzi wengi pamoja na mkuu wa chuo Dokta Swalehe Kaadhim Ajiil na Mheshimiwa Rais kitengo cha athari Ustadh Kaadhim pamoja na idadi kubwa ya wakufunzi wa chuo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: