Kwa ushiriki mkubwa wa kieneo na kiarabu: mchujo wa kaswida zitakazo shiriki katika mashindano ya kongamano la Rabiu Shahada wakamilika…

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada, imetangaza kukamilika mchujo wa kaswida na mashairi yatakayo shiriki katika mashindano ya kwenye kongamano hilo, ambapo watashiriki washairi wa ndani na nje ya Iraq.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa kamati ya matangazo ya kongamano na rais wa kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Aqiil Abdulhussein Yasiri, amesema kua: “Pamoja ya kua shindano linafanywa kwa mara ya kwanza katika ratiba ya kongamano, lakini limepata mwitikio mkubwa kutoka kwa washairi wa kitaifa na kimataifa, jumla ya washairi walio omba kushiriki wamefika (168), tumewachuja na kubaki (111), ambao kaswida na mashairi yao yamekidhi vikezo (10) vya mashindano haya”.

Akabainisha kua: “Tumefuata masharti yanayo tumika katika mashindano ya kimataifa, ili shindano hili liwe sawasawa na mashindano mengine ya kimataifa, mashairi yamekaguliwa na zaidi ya kamati moja, kwa ajili ya kujiridhisha utekelezaji wa kanuni zilizo wekwa na kamati ya maandalizi, kisha yakawasilishwa katika kamati ya majaji, inayo undwa na wasomi wa sekula waliobobea katika fani ya mashairi na lugha, na wenye uzowefu mkubwa wa ufundishaji na uwandishi, kamati hiyo inawajibu wa kuchagua kaswida kumi bora”.

Yasiri akasisitiza kua: “Siku za mbele tutatangaza majina ya washairi watakao faulu pamoja na kuwatumia matokeo yao, ili waje kushiriki katika vikao vya usomaji wa mashairi vitakavyo fanywa katika siku za kongamano litakalo anza mwanzoni mwa mwezi ujao wa Shabani”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: