Mwezi 25 Rajabu ni siku ya huzuni kwa watu wa familia ya Mtume (a.s) kutokana na kifo cha Imamu Mussa Alkadhim (a.s).

Maoni katika picha
Mwezi ishirini na tano Rajabu katika kila mwaka huwa ni siku ya huzuni kwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s) na wafuasi wao kote Duniani, kutokana na kumbukumbu ya kifo cha Imamu wa saba Mussa Alkaadhim bun Jafari Swadiq (a.s), na kukumbuka mateso aliyo pewa na matwaguti miongoni mwa watawala wa bani Abbasi –laana iwe juu yao-.

Jina na nasaba yake (a.s):

Imamu Mussa bun Jafari bun Muhammad bun Ali bun Hussein bun Ali bun Abu Twalib (a.s).

Kuniya yake (a.s):

Abu Hassan, Abu Ibrahim, Abu Ali, Abu Ismail… na ya kwanza ndio mashuhuri Zaidi.

Tarehe ya kuzaliwa kwake (a.s) na mahala alipo zaliwa:

Alizaliwa katika kitongoji cha Abwaau, mwezi 7 Safar mwaka 128h.

Mama yake (a.s) na mke wake.

Mama yake anaitwa Ummu Hamida Barbariyya alikua kijakazi, na mke wake anaitwa bibi Tuktum mama wa Imamu Ridhwa (a.s) alikua kijakazi pia.

Umri wake (a.s) na kipindi cha uongozi wake:

Wakati anauwawa alikua na miaka 55, na kipindi cha Uimamu wake ni miaka 35.

Watawala wa zama zake:

Abu Jafari Mansuur maarufu kwa jina la Dawaniiqi, alikua bahili sana na mpenda mali, neno Dawaniiqi ni wingi wa neno Daaniq, lenye maana ya hela ndogo zaidi katika zama zake, yeye alikua anapenda kukusanya pesa hizo (mzee wa chenchi), Muhammad Mahadi, Mussa Alhaadi, Haruna Abbasiy.

Kufungwa kwake (a.s):

Haruna Abbasiy aliamuru afungwe Imamu Alkaadhim (a.s), kisha akawa anamuhamisha jela moja hadi nyingine, hadi akamuingiza katika jela ya Sindi bun Shaahik aliyekua hana huruma katika moyo wake, na asiyekua na ubinaadamu, alikua haamini akhera, wala hatarajii chochote kwa Mwenyezi Mungu, akampa Imamu (a.s) kila aina ya mateso, akampunguzia chakula na maji ya kunywa, akamfunga minyororo, inasemekana kuwa alimfunga minyororo thelathini ya chuma.

Imamu (a.s) kama kawaida yake alizidisha kufanya ibada, muda mwingi aliutumia kwa kuswali na kusoma Quráni na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumpa faragha ya kufanya ibada.

Barua yake (a.s) kwa Haruna:

Imamu (a.s) alimtumia barua Haruna Abbasiy isemayo kua: (Hakika haipiti siku ya mateso kwangu ispokua inapita kwako siku ya raha, na sote tutakutana katika siku isiyokua na mwisho, na hapo atapata hasara aliyefanya maovu).

Amesema kweli katika barua hakika maumivu yote aliyopata Imamu (a.s) akiwa jela, lazima Twaghuti Haruna Abbasiy atahukumiwa mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu katika siku ambayo waovu watapata hasara.

Sababu ya kifo chake (a.s):

Haruna alimwagiza Sindi amuuwe Imamu (a.s), akamuwekea sumu kali kwenye tende, halafu Sindi akamwambia Imamu azile, Imamu (a.s) akala tende kadhaa, Sindi akamwambia: ongeza, Imamu akaendelea kula hadi Sindi akamwambia: (inatosha, umefikia kiwango unacho hitaji), sumu ikaanza kudhoofisha mwili wake (a.s), akaanza kusikia maumivu makali, Sindi akawa karibu nae kwa ajili ya kuzuwia asitibiwe ili afe haraka.

Kuzikwa kwake (a.s):

Watu wa tabaka zote walitoka kwenda kumzika Imamu Kaadhim (a.s), wakatoka wafuasi wake wakiwa wanajipiga vifua na kububujikwa machozi, washindikizaji wa jeneza lake walijaa katika barabara za Bagdad wakielekea katika eneo la Baabu Tiin wakiwa wamejaa huzuni, wakaenda hadi katika makaburi ya Makuraishi ya Bagdad, wakachimba kaburi lake tukufu na kumzika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: