Wanatuma rambirambi zao katika malalo yake: Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wanampa pole mjikuu wa ndugu yake katika kumbukumbu ya kifo chake.

Maoni katika picha
Mwenyezi Mungu ayakuze malipo yako. Mwenyezi Mungu ayakuze malipo yako ewe Rasulu Llah. Mwenyezi Mungu ayakuze malipo yako ewe kiongozi wa waumini na ewe Fatuma Zaharaa. Mwenyezi Mungu ayakuze malipo yako ewe kiongozi wetu wa zama hizi.

Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), wametuma rambirambi kwa Baqiyatu-Llahi fii Ardhihi na hoja kwa waja wake Imamu wa zama hizi (a.f), kutokana na kifo cha babu yake Imamu Mussa Alkaadhim (a.s).

Wamesimama kwa mstari na kukumbuka yaliyo msibu Imamu Alkaadhim (a.s) katika siku kama ya leo mwezi ishirini na tano Rajabu, wakajikumbusha pia matatizo aliyo pitia katika kipindi chote cha Uimamu wake tangu kifo cha baba yake Imamu Swadiq (a.s), ambapo aliishi katika mazingira magumu sana, kisha Haruna Abbasiy aliyekua unajulikana wazi uadui wake dhidi ya Maimamu wa nyumba ya Mtume (a.s) na wafuasi wao akaamua kumtenga Imamu (a.s) mbali na watu, akamfunga katika jela zenye giza nene, alianza kumfunga katika jela za Basra na akawa anamuhamisha katika jela tofauti hadi alipo mfunga katika jela ya mwisho iliyokua ikisimamiwa na Sindi katika mji wa Bagdad, akaamrisha afungwe minyororo thelathini, ambayo aliendelea kufungwa hadi umauti ulipo mfika kwa kupewa sumu.

Matukio haya yamewafanya watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) watume rambirambi wakiwa na majonzi makubwa ya msiba huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: