Usiku wa simanzi na huzuni katika mji mtukufu wa Kadhimiyya, kama kawaida kila mwaka wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) huhuisha mapenzi na utiifu wao kwa Imamu Kaadhim (a.s), husimama kwa unyenyekevu na kuitikia wito wa kiongozi wao mdhulumiwa aliye uwawa kwa sumu mlango wa haja (baabu hawaaiji) (a.s), wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wamejaa huzuni kubwa katika usiku wa kumbukumbu ya kifo cha Imamu Mussa bun Jafari (a.s).
Kamera ya mtandao wa Alkafeel inakuletea baadhi ya picha za waombolezaji hao.