Kwa sauti ya unyonge na huzuni: watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wanaita waa Kaadhimaahu waa Imamaahu waa Masmumaahu.

Maoni katika picha
Kwa huzuni kubwa Alasiri ya Jumanne (25 Rajabu) sawa na (2 April 2019m) Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimefanya matembezi ya pamoja, kuomboleza kifo cha Imamu Mussa bun Jafari (a.s).

Matembezi yalianzia katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) walisimama kwa mistari huku wakiimba kaswida na mashairi yanayo elezea msiba huo unao umiza roho zao na roho za waumini na wafuasi wa Ahlulbait (a.s), kisha wakaenda katika malalo ya bwana wa mashahidi, wakipitia eneo ya katikati ya haram mbili tukufu huku wanaimba kaswida za huzuni na kulia, kutokana na mazingira ya kuuwawa kwa Imamu wa saba Mussa Alkaadhim (a.s).

Walipo karibia haram ya Imamu Hussein (a.s) wakapokelewa na ndugu zao watumishi wa Atabatu Husseiniyya tukufu, wakajumuika pamoja katika huzuni na wakaingia katika malalo ya Imamu Hussein (a.s) na kufanya majlisi ya kuomboleza, wakaimba kaswida na mashairi ya huzuni pamoja na kuhuisha utiifu kwa Imamu wao na kuahidi kufuata mwenendo wake, na kuchukua mazingatio katika mwenendo wake na mapambano yake matukufu.

Fahamu kua siku ya (25 Rajabu) ni siku ya kukumbuka kifo cha Imamu Mussa Alkaadhim (a.s), waumini wote miongoni mwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika kila sehemu ya dunia huomboleza msiba huu, malalo ya Imamu Alkaadhim (a.s) huko Bagdad imefurika mamilioni ya mazuwaru kutoka ndani na nje ya Iraq kwa ajili ya kuomboleza kifo chake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: