Nyoyo zinanyanyua jeneza lako kabla ya mikono.. ushindikizaji wa jeneza la kuigiza la mtawa wa gerezani Imamu Mussa bun Jafari Alkaadhim (a.s).

Maoni katika picha
Huzuni imetanda katika mbingu ya Kadhimiyya, kutokana na kuteswa kwa mfungwa mdhulumiwa, mamilioni ya mazuwaru wamemiminika kuja kumpa pole Mtume (s.a.w.w) na watu wa nyumbani kwake watakasifu, maneno ya huzuni na vilio yanasikika katika anga, ni vilio juu ya vilio.

Mji mtukufu wa Kadhimiyya asubuhi ya Jumanne mwezi ishirini na tano Rajabu mwaka (1440h) sawa na (2 April 2019m) umeshuhudia matembezi ya kushindikiza jeneza la kuigiza la mtawa wa jela Imamu Mussa bun Jafari Alkaadhim (a.s), matembezi hayo yalikua yanaelekea katika haram tukufu ya Kadhimiyya, na yakapokelewa na watumishi wa Maimamu wawili Aljawaadaini (a.s), huku washindikizai wakiwa ni mamilioni ya watu kutoka ndani na nje ya Iraq.

Katika matembezi hayo kilisomwa kisa cha kuuwawa kwa Imamu Mussa Alkaadhim (a.s) kwa sauti ya Shekh Ahmadi Rabiíy, yakahitimishwa kwa kusoma kaswida na mashairi ya kuomboleza na mtumishi wa Maimamu wawili Aljawadaini (a.s) bwana Karaar Kaadhimiy pamoja na kusoma ziaya ya Imamu Mussa bun Jafari (a.s), na mwisho kabisa ikasomwa dua ya kuwaombea mazuwaru wa Maimamu wawili Aljawadaini (a.s) warudi salama majumbani kwao sambamba na kuliombea amani na utulivu taifa la Iraq, na Mwenyezi Mungu awalinde wanaeshi wetu na Hashdi Shaábi watukufu na awape ushindi daima.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: