Kamati ya maandalizi ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada ya kumi na tano yatangaza ratiba ya kongamano

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada ya kumi na tano linalo ratibiwa na kusimamiwa na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya imetangaza ratiba ya kongamano litakalo fanyika (3-7 Shabani 1440h) kwa ajili ya kuadhimisha kuzaliwa kwa mjjukuu wa Mtume (s.a.w.w), Imamu Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi na Imamu Sajjaad (a.s), chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Hussein –a.s- ni mnara wa umma na mrekebishaji madhubuti).

Ratiba itakua kama ivuatavyo:

Kwanza- Hafla ya ufunguzi, siku ya Jumanne ya mwezi tatu Shabani 1440h, sawa na (9/4/2019m) ndani ya haram tukufu ya Imamu Hussein saa tisa na nusu Alasiri.

Pili- Vikao vya usomaji wa Quráni.

Tatu- Mada za kitafiti za kihauza na kisekula.

Nne- Vikao vya usomaji wa mashairi ya kiarabu fasaha (kwa ushiriki wa washairi wa ndani na nje ya Iraq).

Tano- Vikao vya usomaji wa mashairi ya Shaábi (kwa ushiriki wa washairi wa sha’biyyina).

Sita- Tenzi na kaswida za kidini.

Saba- Kutembelea miradi ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.

Nane- Maonyesho ya vitabu na cd (kwa ushiriki wa taasisi na vituo vya usambazaji wa vitabu vya ndani na nje ya Iraq).

Tisa- Program maalumu ya wageni wanaoshiriki katika kongamano ndani na nje ya Ataba mbili tukufu.

Kumi- Miongoni mwa program za kongamano kuna nadwa ya wanawake.

Kumi na moja- Hafla ya ufungaji siku ya Jumamosi mwezi saba Shabani 1440h.

Fahamu kua baadhi ya vipengele katika ratiba hiyo vinafanyika kipindi chote cha kongamano kama vile maonyesho ya vitabu, na vingine vimegawanywa katika siku za kongamano.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: