Mtume (s.a.w.w) aliletewa ujumbe wa Utume miaka (13) kabla ya kuhama Maka na kwenda Madina, ulikua mwaka wa (610m), Mwenyezi Mungu alimshushia wahyi kupitia Jibrilu (a.s), akamwambia kua yeye ni wa mwisho katika Manabii na Mitume, kutelemka kwa wahyi na kupewa Utume (s.a.w.w) likawa tatizo kwa wajinga, lilikua tatizo la kifikra na kiitikadi, lilikua jambo gumu kueleweka, lakini kuhusu watu walio amini ujumbe wake na wakasadikisha ayasemayo hawakushangazwa na wahyi, walimwamini kutoka ndani ya nafsi zao na kwa msaada wa Mola wao, waliuamini ujumbe wa Mwenyezi Mungu mtukufu uliokuja kumwokoa mwanadamu kutokana na ujinga upotevu na ukatili, kwa sababu Mwenyezi Mungu mtukufu hakumuumba Mwanaadamu bila lengo na wala hakumtelekeza, bali ameleta wahyi ili ajitambulishe kwa mwanaadamu na ajulikane, na mwanaadamu aweze kufikia utukufu duniani na akhera, pamoja na kutoa mwongozo wa namna ya kuishi na watu katika jamii.
Maandalizi ya utume:
Mwenyezi Mungu alimwandaa mtume wake (s.a.w.w) ili aweze kubeba ujumbe wa uislamu ambao ni amana kubwa, na namna ya kuutekeleza, kuwaokoa wanaadamu katika upotevu na ujinga, alipo fikisha (s.a.w.w) umri wa miaka arubaini Mwenyezi Mungu alimteua kuwa Mtume mwenye kulingania watu kwa idhini yake na kuwa sawa na taa liangazalo, alipokua mwishoni mwa kumi la tatu katika umri wake (s.a.w.w) alikua anapata wahyi kwa njia ya ilham na ndoto za kweli, nazo ni miongoni mwa hatua za Utume, kisha Mwenyezi Mungu akaamua kumliwaza na kumuondoa katika upweke, kwani alikua anaenda katika pango (Gharul Hiraa) kufanya ibada, alikua anajitenga na mazingira ya kawaida, na anazama katika kutafakari ukuu wa Mwenyezi Mungu na kujielekeza kwa Mola wake wa pekee.
Kushuka kwa wahyi:
Alipo fikisha umri wa miaka arubaini aliijiwa na Jibrilu (a.s) katika mwezi wa Ramadhani ndani ya siku ya Lailatul Qadri, akamshushia wahyi na kumwambia kuwa yeye ni Nabii na Mtume wa mwisho, na kwamba yeye ametumwa kuwa rehema kwa walimwengu, riwaya zinasema kua aya ya kwanza aliyo soma Jibrilu (a.s) kumfundisha Mtume (s.a.w.w) ni: (Soma kwa jina la Mola wako ambae ameumba…), baada ya Mtume (s.a.w.w) kupokea maelekezo ya Mwenyezi Mungu mtukufu alirudi nyumbani katika familia yake, akiwa amebeba jukumu kubwa, amana ya mbinguni hapa ardhini aliyokua anaisubiri, alipo fika nyumbani akalala na akajifunika shuka huku akiwa anatafakari jukumu alilo pewa, Jibrilu akaja tena kwa mara ya pili na akamtaka aache kulala na aende akaanze kazi ya kulingania watu, Jibrilu alimwambia: (Ewe uliye jifunika maguo * Simama ukaonye..).
Akasimama na kuanza kutekeleza jukumu alilopewa na Mwenyezi Mungu mtukufu, mtu wa kwanza aliye mlingania ni mke wake bibi Khadija (a.s) na mtoto wa Ammi yake Ali bun Abu Twalib (a.s) akiwa na umri wa miaka kumi, wakamwamini na kumsadikisha, wakawa ndio watu wa kwanza katika uislamu, kisha ikashuka amri nyingine ya Mwenyezi Mungu pale alipo sema: (Waonye ndugu zako wa karibu), akawakusanya na akawafikishia ujumbe, aliendelea kulingania Dini hadi mwisho wa uhai wake.
Ibada za siku ya Mab’ath:
Tunapenda kuwakumbusha waumini kuwa, kuna ibada zimesuniwa kufanywa katika usiku wa Mab’ath, miongoni mwa ibada hizo ni:
- -
- - Kuna swala maalumu.
- - Kufunga, nayo ni moja ya siku nne zilizo sisitizwa kugunga ndani ya mwaka.
- - Kumswalia sana Mtume Muhammad na Aali zaje
- - Kumzuru Mtume (s.a.w.w) na kiongozi wa waumini (a.s).
Na zingine nyingi kama zilivyo tajwa katika kitabu cha Mafaatihu Jinaani kilicho andikwa na Shekh Abbasi Qummiy (r.a).