Mwezi 28 Rajabu Imamu Hussein (a.s) anauaga mji wa babu yake na kuelekea Maka

Maoni katika picha
Imamu Hussein (a.s) ameandika katika moja ya barua zake akieleza sababu za kutoka kwake kua: (Mimi sijatoka kwa shari wala kwa majigambo, wala kwa kufanya uovu au dhulma, hakika nimetoka kwa ajili ya kutafuta islahi katika umma wa babu yangu (s.a.w.w), nataka kuamrisha mema na kukataza maovu, na nifuate mwenendo wa babu yangu na baba yangu Ali bun Abu Twalib).

Mwezi (28) Rajabu mwaka (60h), ndio siku ambayo msafara wa Imamu Hussein (a.s) aliondoka Madina na kuelekea Maka, Imamu (a.s) aliondoka na watu wa nyumbani kwake pamoja na wafuasi wake, ikiwa ni pamoja na wake zake na watoto wake wakiongozana na dada yake Zainabu Alkubra (a.s), walitembea katikati ya jangwa wakahimili vumbi na changarawe chini ya uongozi wa Imamu Hussein (a.s), yote hayo ni kwa sababu ya kukataa kusalim amri mbele ya utawala dhalimu wa kimabavu, huku akikumbuka kuhama kwa baba yake Imamu Ali (a.s) kutoka Maka kwenda Madina, siku aliyo ondoka alifuatana na wakina Fatuma wakikataa kusalimu amri mbele ya Makuraishi, kuhama kwao kulikua tofauti na kuhama kuliko zoweleka, waliondoka usiku wa giza, wakapita njia ngumu, wakawa wanaenda huku Imamu (a.s) anasoma aya hii: (Basi akatoka, naye ana khofu, akiangalia huku na huku. Akasema: Mola wangu Mlezi niokoe na watu madhaalimu).

Kabla ya kutoka kwake katika mji wa Madina alikwenda kutembelea kaburi la babu yake (s.a.w.w) na akamuomba Mola wake mbele ya kaburi hilo, akasema: (Ewe Mola hili ni kaburi la Mtume wako Muhammad (s.a.w.w), na mimi ni mtoto wa binti wa Mtume wako, yamenifika mambo unayo yajua, Ewe Mola! Mimi napenda mema na ninachikia mabaya, nakuomba ewe mwenye utukufu na ukarimu, kwa haki ya kaburi hili na aliye ndani yake, unichakulie kufanya unayo yaridhia na yanayo ridhiwa na Mtume wako).

Abu Mukhannaf anasema kua: (Hussein -a.s- alikwenda katika kaburi la babu yake (s.a.w.w) akalia na kusema: Ewe babu yangu, nimelazimika kuondoka jirani yako bila kupenda, kwa sababu nimekataa kula kiapo cha utii kwa Yazidi mlevi na muovu, akiwa katikati ya kulia akashikwa na usingizi, akamuona babu yake (s.a.w.w) akiwa amemkumbatia kifuani kwake na anambusu katikati ya macho mawili huku anamwambia: Ewe mwanangu ewe kipenzi wangu, nakuona baada ya muda mfupi utalala chini ukuwa umelowa damu yako, umechinjwa katika ardhi iitwayo Kafbala, tena ukiwa na kiu, na maadui wako wanatarajia shifaa yangu, mimi sitawaombea shifaa, ewe mwanangu Hussein, hakika baba yako na mama yako na bibi yako, na kaka yako, na ammi yako, na ammi wa baba yako, na wajomba zako, na mama zako na shangazi zako wamekukumbuka, hakika unadaraja kubwa peponi, hauta ipata ispokua kwa kifo, hakika wewe na baba yako na kaka yako, na ammi yako na ammi wa baba yako ni mashahidi mtafufuliwa kwa pamoja na kuingia peponi kwa shangwe na furaha. Akaamka na akawasimlia watu wa nyumbani kwake, wakalia sana kisha wakajiandaa na safari).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: