Kukata utepe wa ufunguzi wa maonyesho ya vitabu ya kimataifa yanayo fanyika Karbala kwa mwaka wa kumi na tano.

Maoni katika picha
Katika eneo lililo pauliwa ndani ya uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu ikiwa kama sehemu ya mwendelezo wa mafanikio yaliyo patikana katika maonyesho yaliyo pita, Alasiri ya Ijumaa (28 Rajabu 1440h) sawa na (5 April 2019m), umefanywa ufunguzi wa maonyesho ya vitabu ya kimataifa ya mwaka wa kumi na tano, ambayo ni sehemu ya ratiba ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada linalo andaliwa na kusimamiwa na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, litakalo anza mwezi tatu Shabani.

Ufunguzi wa maonyesho ya vitabu umehudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Husseiniyya Mheshimiwa Shekh Abdulmahadi Karbalai (d.i), na makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Abbasi Mussa Ahmadi (d.t), pamoja na wajumbe wa kamati kuu za uongozi za Ataba mbili tukufu na mazuwaru.

Baada ya kukata utepe kama ishara ya kufunguliwa kwa maonyesha, wahudhuriaji wakatembelea meza za maonyesho, kwa ajili ya kuangalia bidhaa zilizopo katika maonyesho ya kumi na tano.

Mkuu wa maonyesho haya Dokta Mustaqu Abbasi Muan ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Maonyesho haya ni miongoni mwa vipengele vya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada, awamu hii itakua ya pekee kimpangilio na aina ya vitu vinavyo onyeshwa, vinahusisha watu wa rika zote katika familia, sambamba na uwepo wa vitabu vya fani zote za elimu kuanzia elimu za sekula na za Dini”.

Akafafanua kua: “Kufanya ufunguzi wa mapema ni kwa ajili ya kutoa nafasi zaidi ya muda wa maonyesho, jumla ya nchi nane zimeshiriki katika maonyesho haya, nazo ni: “Marekani, Lebanon, Tunisia, Misri, Iran, Sirya na Jodan) pamoja na mwenyeji wao Iraq, awamu hii imetimia kila sekta, kamati inayo simamia maonyesho haya imechukua hatua za kuzuwia kitabu chochote kinacho ivunjia heshima Iraq, au kinachochea ubaguzi, au kinashambulia alama za Dini, au kina mambo yasiyo kua ya kimaadili”.

Akasema kua: “Ushiriki wa matawi ulifanywa kwa mawasiliano ya mubashara (moja kwa moja) au kwa kutumia mawakala ambao walikua ni: (shule za kisekula - vyuo vikuu – vituo vya utafiti – vituo vya elimu – vituo vya bidhaa za watoto – taasisi za uzalishaji wa vipindi – vituo vya uchapaji na usambazaji), hali kadhalika kuna ushiriki wa Ataba zote za ndani na nje ya Iraq, sambamba na mazaru zote za kishia na kisuni”.

Hafla ya ufunguzi ilipambwa na maonyesho ya Skaut ya Alkafeel ambayo ipo chini ya kitengo cha watoto na makuzi za Atabatu Abbasiyya tukufu, yaliyo sisitiza umuhimu wa kusoma na kupenda taifa.

Kumbuka kua maonyesho ya vitabu ya kimataifa ni kipengele muhimu katika kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada, ambalo huandaliwa na kusimamiwa na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya tangu kuanzishwa kwake, kama sehemu ya kuadhimisha kuzaliwa kwa mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi na Imamu Sajjaad (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: