Maoni katika picha
Msafara huu ni sehemu ya mfululizo wa misafara ya aina hii inayo fanywa katika mikoa mingine ya Iraq chini ya uratibu wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu na utekelezaji wa viongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji blugedi ya 26 katika Hashdi Sha’abi, kwa kutumia (mawakibu za kutoa misaada na idara za ustawi wa jamii katika mikoa 13 – ofisi kuu ya msafara wa Alwafaa- wawakilishi wa kikosi cha Abbasi, taasisi za kiraia zinazo toa huduma za kibinaadamu – pamoja na wahisani wengine), pamoja na kuwasiliana na: (serikali ya mkoa wa Muthanna, na mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu, na idara ya ustawi wa jamii ya Samawah, wawakilishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) waliopo katika mji wa Samawah, pamoja na taasisi zingine za kiraia).