Kuanza kwa hatua ya nne ya uwekaji wa marumaru katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Maoni katika picha
Mafundi na wahandisi wanaofanya kazi katika mradi wa kuweka marumaru kwenye haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wameingia hatua ya nne ya kazi hiyo, ambapo wanaweka marumaru (upande wa kusini) kwenye eneo la kati ya mlango wa Kibla na Amirulmu-uminina (a.s) –baabu kafi-, baada ya kumaliza kazi zote katika hatua ya tatu, katika eneo lililopo kati ya mlango wa Imamu Mussa bun Jafari (a.s) na mlango wa Imamu Hassan (a.s), ambao ni upande wa magharibi wa haram tukufu.

Hii ni kutokana na maelezo iliyopata mtandao wa Alkafeel kutoka kwa Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh rais wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu, akaongeza kusema kua: “Katika uwekaji wa marumaru, Haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) tumeigawa sehemu tofauti, kwa ajili ya kuto watatiza mazuwaru watukufu, kila sehemu tunayo maliza hufunguliwa na kuhamia sehemu nyingine, tutaendelea kufanya hivyo hadi tutakapo maliza kuweka marumaru katika eneo lote la haram tukufu, kwa namna ambayo zinaendana na mapambo mengine yaliyopo ndani ya Atabatu Abbasiyya na kuifanya iwe na muonekano mzuri wakuvutia”.

Akabainisha kua: “Kazi zinazo fanywa katika hatua hii inayo fanana na hatua zilizo pita inavipengele vingi kama ifuatavyo:

  • - Kutoa marumaru za zamani.
  • - Kuondoa sehemu ya zege ya zamani na kurekebisha sehemu zilizo haribika.
  • - Kuziba mipasuko katika ardhi kwa kutumia vifaa maalumu.
  • - Kuweka zege yenye viwango maalumu kwa ajili ya kuandaa sehemu iweze kuwekwa marumaru, zege hilo linashika vizuri katika ardhi na linavitu vya kuzuwia unyevunyevu.
  • - Kutengeneza tabaka la chuma chini ya zege kwa ajili ya kuweka uimara zaidi.
  • - Kuweka mtandao wa kusambaza maji, mawasiliano na utowaji wa tahadhari, na kuunganisha na uwanja wa haram tukufu kwa ajili ya kuunganishwa na mtambo mkuu wa Atabatu Abbasiyya.
  • - Uwekaji wa marumaru kwa kufuata vipimo maalumu na kuhakikisha inaendana na ile iliyopo katika uwanja wa haram tukufu”.

Akasema kua: “Asilimia kubwa ya kazi za awali katika uwekaji wa marumaru hufanywa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi, wao ni washiriki wakuu katika utekelezaji wa mradi huu, wa uwekaji wa marumaru katika uwanja wa haram au katika maeneo mengine ya haram”.

Kumbuka kua mradi wa kuweka marumaru katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ni mradi unaokamilisha miradi iliyo tangulia, unatekelezwa kwa sababu ya kuharibika kwa marumaru zilizopo sasa kutokana na ukongwe wake, kwani zina zaidi ya miaka (50) jambo ambalo limesababisha zipoteze muonekano wake na kuharibu mandhari ya Ataba, ndipo uongozi mkuu wa Atabati Abbasiyya ukaamua kufanya mradi huu kwa lengo la kupendezesha eneo hili takatifu na kulifanya liweze kuburudisha nafsi za mazuwaru watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: