Majina ya tafiti zilizoshinda katika shindano kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada.

Maoni katika picha
Kamati inayo simamia maonyesho imetangaza tafiti zitakazo shinda katika shindano la kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada awamu ya kumi na tano, litakalo anza (3 -7 Shabani 1440h) chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Hussein –a.s- ni mnara wa umma na suluhisho madhubuti), majina ya walioshinda ni haya yafuatayo:

  • - Ustadh Usama Hamidi Atabi, utafiti wake unasema: (Hisia za kimaumbile kwa Imamu Ali bun Hussein –a.s- samo la kichambuzi).
  • - Ustadhat Haifaa Hussein Ni’mah, utafiti wake inasema: (Misingi mikuu katika kujenga fikra kutokana na dua ya Arafa).
  • - Dokta Amaad Kadhwimiy, utafiti wake unasema: (Ujumbe wa mimbari ya islahi.. somo la kichambuzi katika maelekezo ya Marjaa Dini mkuu kwa makhatibu).

Kamati ikaongeza kua: “Hakika tafiti zilizo omba kushiriki katika shindano asilimia kubwa zilitimiza masharti ya utafiti wa kielimu na nyingi zilikua nzuri, zilielezea sehemu muhimu ya maisha ya Imamu Hussein (a.s), katika kushindanisha na kuchuja tafiti hizo tumetumia vigezo vya kielimu na kisekula, ukweli ni kwamba tafiti zote zimeshinda, kwani zimechangia kutangaza utamaduni wa Husseiniyya, tatizo la mashindano huwa yanahitajika majina machache ya washindi”.

Akabainisha kua: “washiriki wote watapewa vyeti vya ushiriki, tafiti ambazo hazija faulu zitapewa umuhimu mkubwa, na mtafiti atapewa cheti cha ushiriki, pia tafiti hizo zitachapiswa katika kitabu maalumu cha kongamano kitakacho gawiwa katika kongamano la mwaka kesho”.

Kamati ya maandalizi imewataka washindi watatu wa kwanza wahudhurie wafike siku ya Jumamosi (13 April 2019m) Alasiri, kwa ajili ya kupokea zawadi zao kwenye hafla ya kufunga kongamano itakayo fanyika ndani ya Atabatu Husseiniyya tukufu, kwa maelezo zaidi unaweza kupiga simu ifuatayo: (07723628171).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: