Maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu yashiriki katika hafla ya siku ya kimataifa ya nakala kale za kiarabu

Maoni katika picha
Kutokana na kuitikia wito wa chuo kikuu cha kiislamu mkoani Najafu Ashrafu, Maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu imeshiriki katika hafla ya siku ya kimataifa kuhusu nakala kale za kiarabu, iliyo andaliwa na Maahadi ya nakala kale kwa kushirikiana na Maahadi ya nakala kale za kiarabu ya mjini Kairo.

Ujumbe huo umeongozwa na mkuu wa kituo cha kupiga picha Ustadh Swalehe Mahadi Abdulwahabi, ambaye ameongea nasi kua: “Jambo zuri ni kuona kuna wanao tilia umuhimu na kuhuisha turathi za umma huu, wenye maelfu ya turathi ambazo bado nuru yake haijaonekana, tumekuja kushiriki kwenye shuguli hii yenye vipengele vingi kwa ajili ya kuangazia jambo hili, kwa ujumla inalenga kuunganisha nguvu na kuongeza utendaji, katika kufichua hazina ya nakala kale zilizo jaa hapa Iraq na katika ulimwengu wa kiarabu, pia kulikua na muhadhara kutoka kwa mkuu wa kitivo cha elimu za kiislamau katika chuo kikuu cha Najafu Dokta Fatuma Salami (kuhusu nakala kale zilizo hamishwa), hali kadhalika tumefanya mahojiano na baadhi ya watu muhimu pembezoni mwa halfa hiyo, kwa ajili ya kuelezea uzowefu wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika sekta ya kuhifadhi nakala kale. Wakati wa kufunga hafla wajumbe kutoka Atabatu Abbasiyya wakapewa vutabu kama sehemu ya kushukuru kushiriki kwao na kuthamini mchango wao kwenye hafla hii”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: