Atabatu Abbasiyya tukufu na maeneo jirani pamepambwa mamia ya taa za rangi.

Maoni katika picha
Kutokana na kuingia mwezi mtukufu wa Shabani ambao unakumbukumbu za kuzaliwa kwa watu watukufu ambao ni miezi ya Muhammadiyya, Atabatu Abbasiyya tukufu imejiandaa kwa kuweka mapambo mazuri yanayo ingiza furaha katika nyoyo, kitengo cha usimamizi wa kihandisi chini ya Ataba tukufu kupitia idara ya umeme, kimefunga taa nyingi za rangi ndani na nje ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Taa za rangi nzuri za kupendeza zimeenea katika uwanja wa haram tukufu, na kuipendezesha mbingu ya mji huu mtukufu, pia kitengo cha usimamizi wa kihandisi kimeongeza taa zingine ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na juu ya jengo kutokana na kuingia mwezi huu wa Shabani, na kuifanya malalo kua sawa na jua liangazalo mwanga mzuri na kuingiza furaha katika nyoyo za wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika kila sehemu ya dunia kutokana na kumbukumbu ya mazazi haya matukufu.

Fahamu kua taa zinazo zunguka malalo tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) au zile zilizopo ndani yake, hubadilishwa kutokana na matukio ya huzuni au ya furaha, kazi hiyo hufanywa na idara ya umeme ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: