Mimbari ya nuru yafanywa kwenye mkoa wa Qadisiyya katika mji wa Diwaniyya

Maoni katika picha
Kituo cha miradi ya Quráni chini ya Maahadi ya Quráni tukufu ya Atabatu Abbasiyya kwenye mradi wa (mimbari za nuru), kimefanya hafla ya usomaji wa Quráni katika mji wa Diwaniyya kwenye mkoa wa Qadisiyya, na kushiriki wasomaji wa Ataba mbili tukufu pamoja na wengine, chini ya mazingira mazuri ya kiroho, hafla imekua na mwitikio mkubwa wa waumini na wadau wa Quráni, waliokuja kusikiliza Quráni tukufu inayo somwa kwa mahadhi mazuri na sauti murua.

Walio burudisha masikio ya wahudhuriaji ni wasomaji wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, bwana Osama Karbalai na msomaji wa Atabatu Abbasiyya Muhammad Ridhwa Salmaan, Sayyid Ali Sharifiy na Mauhubu Tammaar Muhammad.

Kumbuka kua miongoni mwa miradi ya Quráni endelevu, ni mradi wa mimbari za nuru, ambao ni kufanya mahafali za vikao vya kusoma Quráni ndani na nje ya mkoa wa Karbala, na katika Ataba tukufu au mazaru takatifu, na katika Husseiniyya na misikiti, na hushiriki wasomaji wa ndani na nje ya Iraq, kwa kufuata ratiba maalumu inayo lenga kufundisha umuhimu wa kushikamana na kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu, kwa kufanya miradi mbalimbali ya usomaji wa Quráni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: