Maonyesho ya vitabu ya kimataifa yanayo fanyika Karbala ni jicho la wakufunzi wa vyuo vikuu

Maoni katika picha
Idara ya mahusiano na vyuo vikuu chini ya kitengo cha mahusiano cha Atabatu Abbasiyya tukufu, imeratibu matembezi ya jopo la wakufunzi wa kemia katika kitivo cha sayansi kwenye chuo kikuu cha Bagdad katika korido za maonyesho ya vitabu ya kimataifa yanayo fanyika Karbala, katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu lililo pauliwa.

Matembezi hayo wamefanywa baada ya idara tajwa hapo juu kupokea wageni kutoka kwenye chuo kikuu cha Bagdad, ambao ni wakufunzi na wanafunzi, waliokuja kutembelea maonyesho haya, ya kumi na tano. Ilikua ni fursa muhimu kwao kuangalia vitabu vinavyo kidhi mahitaji yao kielimu.

Rais wa kitengo cha kemia katika kitivo cha sayansi/ kwenye chuo kikuu cha Bagdad Dokta Nasoro Dhiyaau Sha’alani baada ya kumaliza matembezi yao ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Tunaishukuru sana Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana kwake na taasisi za kisekula pamoja na vyuo vikuu, kwa kufanya program mbalimbali, hata ziara yetu ni miongoni mwa harakati zake”.

Akaongeza kua: “Maonyesho ya vitabu ya Karbala yamejaa elimu mbalimbali, idara ya maonyesho haijasahau elimu za sekula na vyuo vikuu, imezipa nafasi kubwa kwa kiasi inakidhi mahitaji ya wanachuo na wahadhiri wao, matembezi yetu yanafaida kubwa sana, tutatembelea tena maonyesho haya kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mtukufu, tunazishukuru sana Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kwa utaradibu mzuri walio weka, pia tunawashukuru sana wasimamizi wa maonyesho haya”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: