Kuzaliwa kwa Imamu Hussein (a.s) kuliwasha taa la uongofu na kung’oa nanga ya safina ya uokovu

Maoni katika picha
Katika siku kama ya leo mwezi tatu Shabani mwaka wa nne hijiriyya, alizaliwa Imamu Hussein (a.s), kwa ujauzito wa miezi sita akiwa msafi mtakasifu, hakuna aliyezaliwa akiwa na miezi sita ispokua Nabii Issa mwana wa Maryam na Hussein (a.s), Mtume (s.a.w.w) akamwita shangazi yake Sofiya: (Ewe shangazi yangu niletee mwanangu) Sofia akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu hatuja msafisha, akasema (s.a.w.w): (Ewe shangazi yangu, wewe ni wa kumsafisha?! Hakika Mwenyezi Mungu mtukufu amesha msafisha na kumtwaharisha).

Katika riwaya nyingine inasema: Mtume (s.a.w.w) alikwenda katika nyumba za Zaharaa (a.s), akaomba apewe mtoto wake Hussein, Asmaa bint Umais akamletea, Mtume (s.a.w.w) akamchukua na kumuadhinia katika sikio la upande wa kulia na akakimu katika sikio la kushoto, wakati anafanya hivyo, Jibrilu (a.s) akaja na akamwambia Mtume (s.a.w.w) jina la mtoto huyu ni “Hussein”, kisha akasikika Mtume (s.a.w.w) analia, Asmaa akauliza sababu ya kulia wakati amejaliwa mtoto mtukufu, akamwambia kua Jibrilu kaniambia; watu waovu watamuua katika ardhi inayo itwa Karbala, na akamtaka asimwambie Fatuma (a.s).

Siku ya saba tangu kuzaliwa kwake, Mtume (s.a.w.w) akamfanyia hakika, kwa kuchinja mbuzi na kumnyoa nywele kisha akatoa sadaka ya fedha kwa uzito wa nywele zile na akaamuru afanyiwe sunna (atahiriwe). Shekhe Kuleini (q.s) katika kitabu cha Kafi, anasema kua; alikua analetwa kwa Mtume (s.a.w.w) anamuwekea kidole gumba chake mdomoni, ananyonya na anashiba kwa muda wa siku mbili hadi tatu, mwili wa Imamu Hussein ukajengeka kutokana na Mtume (s.a.w.w), hakuna aliyezaliwa (akiwa kamili) kwa ujauzito wa miezi sita ispokua Nabii Issa mwana wa Maryam na Hussein bun Ali (a.s). kitabu Alkaafi/ mlango wa kuzaliwa kwa Hussein (a.s).

Mtume (s.a.w.w) aliingiza ukarimu na utukufu wake kwa Imamu Hussein (a.s) ili awe ni mwendelezaji wa malengo yake na mwenye kuhami misingi yake.

Imamu Hussein (a.s) alikua anafanana na babu yake Mtume (s.a.w.w), alikua anafanana nae kwa sura sambamba na kufanana nae kwa tabia njema ambazo aliwashinda Mitume wote. Imamu Ali (a.s) anasema: (Anayetaka kumwangalia mtu anaefanana zaidi na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kuanzia shingoni hadi kiunoni kwake, amwangalie Hussan, na anaetaka kumwangalia mtu anayefanana zaidi na Mtume (s.a.w.w) kuanzia shingoni hadi kwenye unyayo kimaumbile na rangi amwangalie Hussein bun Ali).

Katika uso wake mtukufu alikua na siri za Uimamu, alikua na uso mzuri zaidi, alikua kama anavyo sema Abu Kabiri Hadhaliy: ukiangalia uso wake ulikua unametameta, baadhi ya waandishi wanasema: alikua na uso mweupe hata akikaa katika sehemu yenye giza mwanga wa uso wako unamuongoza, wengine wanasema, alikua na uzuri wa ajabu, nuru ilikua inawakawaka katika uso wake na mashavu yake yalikua yanatoa mwanga katika usiku wa giza, alikua anafanana zaidi na Mtume wa Mwenyezi Mungu, baadhi ya mashahidi katika wafuasi wake waliimba beti za kumsifu wakisema:

Mwanga wake huchomoza kama jua la dhuha, na nuru yake huangaza kama mwezi ya badri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: