Shule ya sekondari ya Almaqaaswid yatoa zawadi kwa wanafunzi wake walio fanya vizuri ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Uongozi wa shule binafsi ya sekondari Almaqaaswid umeamua kuwapa zawadi ndani ya Atabatu Abbasiyya wanafunzi wake walio fanya vizuri, kwa ajili ya kutaka baraka za mwenye malalo hii Abulfadhil Abbasi (a.s), wanafunzi na viongozi wa shule hiyo wamepokelewa na watumishi wa idara ya mahusiano na vyuo vikuu ya Ataba tukufu.

Baada ya kufanya ziara tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ugeni wa shule ya Almaqaaswid pamoja na wanafunzi wao wakaelekea katika ukumbi wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s), kwa ajili ya kuwapa zawadi wanafunzi wao walio fanya vizuri.

Kumbuka kua shule binafsi ya sekondari ya Almaqaaswid ipo katika mtaa wa Alkaraadah, na ipo chini ya taasisi ya khairiyya ya kiislamu, ilianzishwa mwaka wa 1949m kwa malengo ya kibinaadamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: