Kuhuisha mazazi ya miezi ya Muhammadiyya ndani ya mwezi wa Shabani mazingira ya furaha yametanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Mwezi wa shabani umesha ingia ukiwa na kumbukumbu za mazazi matukufu, mji wa Karbala umejaa furaha kwa kuukaribisha mwezi mtukufu wa Shabani, mazingira ya shangwe na furaha yameenea katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa miezi ya Muhammadiyya Maimamu watakasifu, Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi na mtoto wake Sajjaad (a.s), pamoja na kuzaliwa kwa Imamu wa zama Hujjat bun Hassan (a.f).

Pembezoni mwa uwanja wa haram tukufu kumewekwa vitambaa vilivyo andikwa maneno ya kuonyesha utiifu kwa watukufu hao, kuta na minara yake imepambwa kwa taa za rangi, sambamba na maua ambayo kwa kiasi kikubwa yamependezesha haram tukufu, mazingira ya furaha sio kwamba yapo ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) peke yake, bali yameenea hadi nje katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu hadi katika malalo ya bwana wa vijana wa peponi Abu Abdillahi Hussein (a.s).

Kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimefanya kazi kubwa kuhakikisha kinaweka mazingira ya shangwe na furaha kutokana na utukufu wa mwezi huu wa Shabani.

Fahamu kua mwezi tatu Shabani ni siku aliyo zaliwa bwana wa mashahidi Abu Abdillahi Hussein bun Ali (a.s), na mwezi nne alizaliwa Abulfadhil Abbasi (a.s), na mwezi tano alizaliwa Imamu Ali bun Hussein Zainul-Aabidina (a.s), na mwezi kumi na moja alizaliwa Ali Akbaru bun Imamu Hussein (a.s), na mwezi kumi na tano alizaliwa Baqiyyatu Llahi Swahibu Asri wa Zamaan Imamu Muhammad bun Hassan (a.f).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: