Balozi wa Uturuki nchini Iraq afurahishwa na bidhaa zinazo tengenezwa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika viwanda vyake na mazao yanayo toka kwenye mashamba yake.

Maoni katika picha
Balozi wa Uturuki nchi Iraq ametembelea korido (meza) za Atabatu Abbasiyya tukufu katika maonyesho ya biashara ya kumi na sita ya nchi wanachama wa ushirikiano wa kiislamu, yanayo andaliwa na wizara ya viwanda ya Iraq katika uwanja wa maonyesho ya kimataifa mijini Bagdad.

Balozi wa Uturuki amefurahishwa na bidhaa zilizopo kwenye korido za Atabatu Abbasiyya tukufu, amesifu ubora wa bidhaa za viwandani na mashambani, akasema: “Hakika yanayofanywa na Atabatu Abbasiyya katika sekta ya uchumi na biashara yanamchango mkubwa katika uchini wa Iraq”. Akabainisha kua: “Huduma za Ataba tukufu haziishii katika sekta ya viwanda na kilimo peke yake, bali ni Zaidi ya hapo, wanatoa pia huduma za afya, elimu na zinginezo, bila shaka hii ni taasisi kubwa ya kidini”.

Fahamu kua Atabatu Abbasiyya tukufu inashiriki katika maonyesho ya biashara ya kumi na sita ya nchi wanachama wa ushirikiano wa kiislamu, kupitia matawi yake matatu: viwanda, kilimo na ujenzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: