Angalia kwa picha: Dirisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) limepambwa mauwa na kuwekwa manukato…

Maoni katika picha
Kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Abulfadhil Abbasi (a.s), aliye zaliwa mwezi nne Shabani pamoja na kuzaliwa miezi ya Muhammadiyya (a.s), Atabatu Abbasiyya tukufu imepambwa maua mazuri, na dirisha la kaburi lake tukufu limewekwa maua mazuri yanayo akisi harufu nzuri ya utukufu wake, maua hayo yamewekwa kila sehemu ya haram na kuifanya mandhari kuwa nzuri yenye kuingiza furaha katika nyoyo za waumini kutokana na mazazi haya matukufu.

Yametoka katika vitalu vya Alkafeel na yamewekwa kwa ustadi na umaridadi mkubwa kwa namna ambayo kila mtu anayeingia ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu anahisi amani na utulivu.

Maua haya hayajawekwa ndani ya malalo peke yake, bali yamewekwa hadi nje ya malalo, yamewekwa milangoni na katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, yanampa harufu nzuri kila anayekuja katika kaburi mbili takatifu kwa ajili ya kuadhimisha mazazi haya matukufu.

Kumbuka kua kazi ya kuweka maua ni miongoni mwa sehemu za maandalizi maalumu ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika mwezi huu wa Shabani, kutokana na matukio yanayo patikana katika mwezi huu likiwemo la kuzaliwa Imamu wa zama Hujjat bun Hassan Mahadi (a.f), pamoja na mazani mengine matukufu yaliyo tokea katika mwezi huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: