Kuzaliwa kwa Abulfadhil Abbasi (a.s) ni kuzaliwa kwa uaminifu na undugu na dunia imeangaziwa utukufu wake.

Maoni katika picha
Mwezi nne Shabani ni siku aliyozaliwa Abulfadhil Abbasi mototo wa kiongozi wa waumini (a.s) aliye pewa jina la mwezi wa bani Hashim na muasisi wa utukufu na uaminifu, dunia imeangaziwa na nuru ya kuzaliwa mwezi wa bani Hashim kwa kuchomoza nuru yake tukufu iliyo jaa ujasiri na kulelewa na miguu ya ukhalifa, akalelewa katika nyumba ya Uimamu na utukufu na akawa ni mwenye kuipa nyongo dunia, hakupata tatizo ispokua lilimuongezea Imani na kuimarisha msimamo.

Abulfadhil Abbasi (a.s):

Kuzaliwa kwake kulikua kwa pekee kama ilivyo kwa mawalii wa Mwenyezi Kumgu, kuzaliwa kwake kulijaa maajabu, mambo yaliyo onekana yaliashiria utukufu wake mbele ya Mwenyezi Mungu.

Bishara ya kuzaliwa kwake (a.s):

Abulfadhil Abbasi (a.s) ni mototo wa kwanza wa Ummul-Banina, dunia ilinawirika kwa kuzaliwa kwake, furaha ikajaa katika familia ya Alawiyya, kwa kuzaliwa mwezi wao ungáao, unao angazia mbingu na ardhi, aliwaongezea utukufu bani Hashim na utajo mzuri. Imamu kiongozi wa waumini (a.s) alipo pewa taarifa ya kuzaliwa kwa mototo huyu mtukufu, alikwenda haraka nyumbani kwake, alipo fika akamchukua na kumbusu kwa muda mrefu, akamfanyia utaratibu wa kisheria, akamuadhinia katika sikio la kulia na kukimu katika sikio la kushoto, sauti ya kwanza aliyo sikia ilikua ni sauti ya baba yake kilele cha Imani na taqwa katika ardhi, maneno matakasifu yasemayo. (Allahu Akbaru…), (Laa ilaaha illa Llah).

Maneno hayo matukufu yaliingia katika akili ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na yakawa ndio uhalisia wake, maisha yake yote alijitolea kulingania maneno hayo, na akauwawa kwa ajili ya maneno hayo.

Siku ya saba tangu kuzaliwa kwa Abulfadhil Abbasi (a.s), Imamu kiongozi wa waumini (a.s) alinyoa nywele zake na akatoa sadaka ya dhahabu au fedha kwa uzito wa nywele hizo kwa masikini na kumfanyia hakika kwa kuchinja mbuzi, alifanya sawa na alivyo fanya kwa Hassan na Hussein (a.s).

kupewa kwake jina:

Imamu kiongozi wa waumini (a.s) alimpa jina mwanae la (Abbasi), alitambua kua atakua miongoni mwa makamanda wakubwa katika uislamu, atakua tishio kwa waovu na watenda batili, na furahisho kwa watu wema wafanyao kheri, akawa namna hiyo, alikua jemedari shupavu na tishio kubwa dhidi ya maadui wa Ahlulbait (a.s) katika vita zote alizo shiriki, aliua makomando wao na kuangamiza majeshi yao, baada ya kuingia katika uwanja wa vita wa Karbala wanajeshi wa maadui wote walijaa hofu, mshairi anasema:

Watu walikunja nyuso zao kwa kuogopa kufa ** huku Abbasi akicheka na kutabasamu.

Alikua ni kilele cha utukufu na mfano bora, kwa sababu alinufaika vyema na jua la Uimamu, yeye na ndugu yake Shahidi (a.s) walikua sawa na aya za Quráni zisemazo: (Naapa kwa jua na mwangaza wake * na kwa mwezi unapo lifuatia), kila kauli na kitendo kutoka kwa Hussein (a.s) yeye alikifanyia kazi, alinufaika kwa kufuata mafundisho na mwongozo wake katika kila kitu hadi katika kuzaliwa, Imamu (a.s) alizaliwa mwezi tatu Shabani na Abulfadhil Abbasi akazaliwa mwezi huohuo tarehe nne Shabani mwaka wa ishirini na sita hijiriyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: